Wafuasi wa Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
wamepata ushindi mkubwa katika uchaguzi wa majimbo ambapo kati ya
majimbo 19 wamepata ushindi katika majimbo 14.
Shirika la habari la Reuters limeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa,
tume ya uchaguzi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imetangaza kuwa,
viti vya majimbo hayo matano yaliyosalia vimechukuliwa na wagombea huru,
na uchaguzi wa jimbo moja umeingia katika duru ya pili.
Wapinzani wanalalamikia matokeo hayo wakisema kuwa wafuasi wa Rais
Joseph Kabila wamepata ushindi mkubwa katika uchaguzi huo kutokana na
nguvu za vyombo vya dola na uchakachuaji wa matokeo.
Matokeo ya uchaguzi huo yamemuongezea nguvu Rais Kabila na kutoa
uwezekano wa kuendelea urais wake kwa kipindi kingine hasa kwa
kuzingatia kuwa wafuasi wake wanaendesha kampeni za kubadilisha katiba
ili imruhusu kuendelea kugombea urais katika uchaguzi ujao.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269