Na Anita Jonas-Maelezo
Dar es Salaam.
Kaimu
Mkurugenzi Jiji la Dar es Salaam Bi. Sara Yohana amemtanganza Diwani wa Kata ya Vijibweni, Manispaa ya Temeke (CHADEMA), Isaya Chacha Diwani kuwa Meya Mpya wa Jiji hilo.
Kaimu
Mkurugenzi huyo alimtangaza Isaya kuwa mshindi mwishoni mwa uchaguzi uliofanyika leo, na diwani huyo kuibuka mshindi kwa kupata kura
84 dhidi ya mgombea kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Yenga Yusuph
ambaye alipata kura 67 wakati kura 7 ziliharibika katika uchaguzi huo.
“Tunawashuruku
wapiga kura wote mlioshiriki zoezi hili la upigaji kura kwa utulivu
bila vurugu na kuweza kufanikisha mpaka kumpata Meya wa Jiji hili”
alisema Bi Yohana.
Kwa
upande wa mshindi wa Kiti cha Meya wa Jiji Mhe. Chacha aliwashukuru
wapiga kura wake wa kata ya Vijibweni kwa kumchagua kuwa Diwani pamoja
uongozi wa chama chake kukubali kumpa nafasi ya kugombea kiti hicho cha Umeya.
“Nimejipanga
kuleta maendeleo katika sekta ya elimu pamoja na kupambana na kero ya
foleni katika jiji letu na nitahakikisha wananchi wote maskini
wanafaidika na mapato ya jiji hili ikiwemo kuendeleza miundombinu
mbalimbali ,”alisema Chacha.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269