Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza umuhimu wa
kuimarishwa ushirikiano kati ya Tehran na Islamabad katika nyuga
mbalimbali hususan katika vita dhidi ya ugaidi.
Akihutubia waandishi wa habari katika mji mkuu wa Pakistan,
Islamabad, Rais Hassan Rouhani alisema nchi mbili hizo zimeafikiana
kushirikiana katika kuzima harakati za makundi ya kigaidi yanayotishia
usalama katika mipaka ya nchi hizo; mashariki mwa Iran na magharibi mwa
Pakistan. Rais Rouhani ameongeza kuwa uhusiano wa Iran na Pakistan ni
muhimu na kusisitiza kuwa, nchi mbili hizo zina mambo mengi
yanayoziunganisha pamoja, yakiwemo ya kidini, kihistoria na kiutamaduni.
Kwa upande Waziri Mkuu wa Pakistan, Nawaz Sharif amesema taifa lake
linajivunia uhusiano mzuri na wa muda mrefu na Iran na kwamba, mkutano
kama huu wa Islamabad ni wa tatu katika kipindi cha miaka zisizozidi
mitatu.
Ameashiria kuwa kikao chake na Rais Rouhani mjini Islamabad kimegusia
masuala mbali mbali yakiwemo ya kieneo na kwamba pande mbili hizo
zimesaini makubaliano kadhaa katika nyuga tofauti kama vile ya
kibiashara, sekta ya uchukuzi na nishati.
Ni vyema kuashiria hapa kuwa, Waziri Mkuu wa Pakistan aliitembelea Iran Januari 19 mwaka huu.
Wakati tunaenda mitamboni, Rais wa Iran na Waziri Mkuu wa Pakistan walikuwa wanahutubia mkutano wa kibiashara mjini Islamabad.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269