MRATIBU WA MASHIRIKA YA UMOJA WA MATAIFA HAPA NCHINI AMTEMBELEA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI.
Mwakilishi
Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo ambaye pia
ni Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa hapa nchini Bw. Alvaro
Rodriguez akimweleza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi nia ya Mashirika
hayo ya kuisaidia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi katika masuala
mbalimbali. Bw. Rodrequez alimtembelea Mhe. Kitwanga ofisini kwake leo.
Kushoto ni Afisa wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo
(UNDP) Bi. Gertrude Lyatuu.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Charles Kitwanga akimwelezea Mratibu
wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa (UN) hapa nchini Bw. Alvaro Rodriguez
(katikati) mipango ya Wizara yake ambayo inaweza kusaidiwa na Mashirika
ya Umoja wa Mataifa hapa nchini. Bwana Rodriguez alimtembelea Mhe.
Kitwanga ofisini kwake leo kuelezea nia ya Mashirika hayo ya kuisaidia
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Kushoto ni Afisa wa Shirika la Umoja
wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP) Bi. Gertrude Lyatuu.
Mwakilishi
Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo ambaye pia
ni Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa hapa nchini Bw. Alvaro
Rodriguez akimwonyesha Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Charles
Kitwanga mojawapo ya makabrasha ya Mashirika hayo yenye mipango ya
maendeleo ya kuisaidia Tanzania. Bw. Rodriguez alimtembelea Mhe.
Kitwanga ofisini kwake kuelezea nia ya Mashirika ya Umoja wa Mataifa ya
kuisaidia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi katika kutekeleza baadhi ya
majukumu yake. Kushoto ni Afisa wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango
wa Maendeleo (UNDP) Bi. Gertrude Lyatuu.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Charles Kitwanga akisisitiza jambo
kuhusiana nia ya Mashirika ya Umoja wa Mataifa ya kuisaidia Wizara yake.
Katikati ni Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa yaliyoko hapa
nchini Bw. Alvaro Rodriguez aliyemtembelea Mhe. Kitwanga ofisini kwake
leo kuelezea nia ya Mashirika hayo ya kuisaidia Wizara ya Mambo ya Ndani
ya Nchi. Kushoto ni Afisa wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa
Maendeleo (UNDP) Bi. Gertrude.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Charles Kitwanga akimshukuru Mratibu wa
Mashirika ya Umoja wa Mataifa yaliyoko hapa nchini Bw. Alvaro Rodrigues
kwa kueleza nia ya Mashirika hayo kutaka kuisaidia Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi. Bw. Rodrequez alimtembelea Mhe. Kitwanga ofisini kwake
leo. Kushoto ni Afisa wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa
Maendeleo (UNDP) Bi. Gertrude Lyatuu.
(PICHA ZOTE NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI– WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI).
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269