Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph
Magufuli (kulia) akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia, Adel Al Jubair alipowasili nchini kwa ziara ya siku moja. Wakati
wa ziara hiyo Mhe. Al Jubair alipata fursa ya kufanya mazungumzo na
Rais Magufuli pamoja na kusaini Mkataba wa Ushirikiano kati ya Tanzania
na Saudi Arabia katika nyanja za Uchumi, Biashara, Uwekezaji, Vijana na
Michezo. Waziri Al Jubair pia alimfikishia Rais Magufuli salamu kutoka
kwa Mfalme Salman wa Saudi Arabia.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph
Magufuli pamoja na wajumbe wa Serikali zote mbili wakishuhudia uwekwaji
saini wa mkataba kuhusu Ushirikiano kati ya Tanzania na Saudi Arabia
katika nyanja za Uchumi, Biashara, Uwekezaji, Ufundi, Vijana na Michezo.
Kwa upande wa Tanzania mkataba ulisainiwa na Waziri wa Mambo ya Nje,
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustine
Mahiga (kulia) na Serikali ya Saudi Arabia iliwakilishwa na Waziri wa
Mambo ya Nje, Adel Al Jubair.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph
Magufuli pamoja na wajumbe wa Serikali zote mbili wakishuhudia
kubadilishana hati baada ya uwekwaji saini wa mkataba kuhusu Ushirikiano
kati ya Tanzania na Saudi Arabia katika nyanja za Uchumi, Biashara,
Uwekezaji, Ufundi, Vijana na Michezo. Kwa upande wa Tanzania mkataba
ulisainiwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustine Mahiga (kulia) na Serikali ya
Saudi Arabia iliwakilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Adel Al Ju
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli (kulia) akiwa katika mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia, Adel Al Jubair alipowasili nchini kwa ziara ya siku moja. Wakati wa ziara hiyo Mhe. Al Jubair alipata fursa ya kufanya mazungumzo na Mhe. Rais Magufuli pamoja na kusaini Mkataba wa Ushirikiano kati ya Tanzania na Saudi Arabia katika nyanja za Uchumi, Biashara, Uwekezaji, Vijana na Michezo. Waziri Al Jubair pia alimfikishia Rais Magufuli salamu kutoka kwa Mfalme Salman wa Saudi Arabia. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia, Al Jubair, Waziri Mahiga, Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje, Balozi Abdallah Kilima (wa kwanza kulia) na ujumbe uliombatana na Waziri Al Jubair.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269