Bomba hilo la lilivunjika kutoka na mvua zinazoendelea kunyesha maendeleo mbali mbali ya nchi katika eneo la Bonde Kihangaiko Msata,aidha ujenzi unatarajiwa kukamilika na kurudisha hali ya upatikanaji wa maji katika hali yake ya kawaida kwa wakazi wa Chalinze.
mafundi wakiendelea na kazi ya ujenzi.
Bweni la Shule ya Sekondari Chalize likiwa limeharibiwa vibaya na moto.
katika hatua nyingine Ridhiwani ametembelea shule ya Sekondari ya Chalinze ambapo Bweni la wavulana liliwaka moto usiku wa kuamkia leo na kusababisha hasara ya mali mbali mbali za wanafunzi wanaishi katika bweni hilo.
Ridhiwani amesema kuwa kwa kushirikiana na wahisani mbali mbali watajenga upya jengo hilo ili kuliweka katika mazingira rafiki kwa wanafunzi,na kutoa msaada wa Magodoro 70,Vitanda,Shuka mbili mbili kwa kila kitanda pamoja na nguo ambazo watakabidhiwa wanafunzi hao.
Mbunge wa Chalinze Ridhiwani aliyeshika kiuno akiangalia jengo hilo lilo teketea kwa moto shuleni hapo
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269