Ndege ya abiria ya shirika la EgyptAir
iliyokuwa imebea abiria 56 na wahudumu 10 wakiwemo marubani imetoweka
kwenye rada, ikitokea mji mkuu wa Ufaransa Paris kuelekea Cairo, mji
mkuu wa Misri.
Gazeti la serikali la Ahram limeripoti kuwa, ndege hiyo yenye
nambari ya usajili A320, ilikuwa inaruka umbali wa mita 11,300 kabla ya
kutoweka kwenye rada, mashariki mwa bahari ya Mediterranean, maili 10
kabla ya kuingia kwenye anga ya Misri. Maafisa wa Idara ya Safari za
Anga nchini Misri wamesema yumkini ndege hiyo imeanguka katika bahari
hiyo.
Kwa mujibu wa Wizara ya Uchukuzi ya Misri, abiria waliokuwa kwenye
ndege hiyo ni pamoja na Wamisri 30, raia 15 wa Ufaransa na Muingereza
mmoja.
Itakumbukuwa kuwa, ndege nyingine ya abiria ya shirika la Metrojet la
Russia nambari A321, ilianguka katika Peninsula ya Sinai nchini Misri
Oktoba 31 mwaka jana, na kuua watu wote 224 waliokuwemo kwenye ndege
hiyo.
Aidha ndege nyingine ya abiria ya shirika la EgyptAir iliyokuwa na
abiria 55 na wahudumu 7 ambayo ilikuwa inatoka Alexandria kwenda jijini
Cairo, ilitekwa nyara na raia wa Misri ambaye aliaminika kuwa na akili
taahira kwa jina Seifuddin Mustafa ambaye alidai kuwa alifanya hivyo ili
kuishinikiza serikali ya Cairo iwaachie huru wafungwa wa kisiasa kabla
ya kubadili kauli yake na kusema kuwa alitaka aletewe mtalaka wake raia
wa Cyprus waonane katika uwanja wa ndege wa kisiwa hicho.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269