Kinara wa upinzani nchini Uganda, Dakta Kizza
Besigye amesema maisha yake yamo hatarini na kwamba yumkini atauawa
katika gereza kuu la Luzira, ambako anazuiliwa kwa sasa.
Besigye aliyasema hayo jana Jumatano alipofikishwa katika
Mahakama ya Hakimu Mkuu Nakawa, ambapo anakabiliwa na tuhuma za uhaini,
kwa kujiapisha kuwa rais wa nchi hiyo, siku moja kabla ya kuapishwa Rais
Yoweri Museveni.
Besigye ambaye alifika mahakama hapo bila wakili, alimwabia Hakimu
James Ereemye kwamba maisha yako yamo hatarini, na haelewi ni kwa nini
alihamishwa kutoka gereza la Moroto na kupelekwa Luzira ambako anadai
anateswa. Hata hivyo Frank Baine, msemaji wa gereza la Luzira baadaye
aliwaamba waandishi wa habari kuwa, kiongozi huyo wa chama cha FDC hafai
kuwa na hofu na kusisitiza kuwa jela za nchi hiyo zina wafungwa zaidi
ya 46,000 na hamna yeyote miongoni mwao anayepatiwa huduma maalum wala
kuhatarishwa maisha. Mahakama hiyo imeagiza kwamba, Besigye asalie
rumande hadi Juni Mosi, wakati ambao kesi hiyo itasikilizwa tena.
Mgogoro wa kisiasa nchini Uganda uliibuka baada ya mirengo ya
upinzani kupinga matokeo yaliyompa ushindi Rais Yoweri Kaguta Museveni
wa nchi hiyo katika uchaguzi uliofanyika mwezi Februari mwaka huu.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269