Spika wa Baraza la Seneti nchini Burundi
ameelezea habari ya safari ya Spika wa Bunge la nchi hiyo, Révérien
Ndikuriyo nchini Morocco katika kukamilisha ushirikiano wa pamoja wa
kibunge baina ya nchini hizo mbili.
Stella Budiriganya, msemaji wa Baraza la Seneti la nchi hiyo
ameviambia vyombo vya habari kwamba, Ndikuriyo alifanya safari nchini
Morocco Jumamosi ya jana katika fremu ya kuimarisha ushirikiano uliopo
kati ya bunge la nchi hiyo na lile la Burundi. Aidha Bi. Stella
Budiriganya ameongeza kuwa, bunge la seneti la nchi Burundi linaisaidia
serikali katika kufanikisha siasa kuu za kitaifa nchini humo. Hii ni
katika hali ambayo, katika safari yake nchini Burundi hapo tarehe 28
Machi mwaka huu, ujumbe wa bunge la Morocco ulisisitiza kuwa
wanaharakati wa kiuchumi wa Morocco watafanya safari hivi karibuni mjini
Bujumbura kwa lengo la kutathmini uwezekano wa kuwekeza katika sekta
tofauti nchini humo. Kadhalika kamati ya bunge la Morocco ilisema kuwa,
shirika moja la ndege la nchi hiyo litaanza kufanya safari za moja kwa
moja baina ya Bujumbura na Casablanca.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269