Breaking News

Your Ad Spot

May 23, 2016

MWENYEKITI WA MTAA WA BABALE ULIOPO WILAYA YA NYAMAGANA AUAWA KWA KUPIGWA RISASI NA WATU WASIOFAHAMIKA WAKATI AKIELEKEA NYUMBANI KWAKE.

msa1
MNAMO TAREHE 22.05.2015 MAJIRA YA SAA 20:00HRS KATIKA MTAA WA BULALE KATA YA BUHONGWA WILAYA YA NYAMAGANA JIJI NA MKOA WA MWANZA, MWENYEKITI WA MTAA WA BUBALE ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA ALPHONCE MUSSA NYINZI MIAKA 48, MSUKUMA MFANYABIASHARA NA MKAZI WA BULALE ALIUAWA KWA KUPIGWA RISASI KIFUANI NA KUTOKEA CHINI YA KWAPA UPANDE WA KULIA NA WATU WAWILI WASIO FAHAMIKA. RISASI HIYO PIA ILIMJERUHI NEEMA MARANGULA MIAKA 23 MKAZI WA BULALE KATIKA KIGANJA CHA MKONO WA KULIA.
 
INAELEZWA KWAMBA SIKU HIYO JIONI ALIKUA AMETOKA KWENYE KIKAO ALICHOFANYA NA WAJUMBE WA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA WA MTAA WA BULALE, KATIKA MUDA WA SAA 20:00HRS USIKU AKIELEKEA NYUMBANI AKIONGOZANA NA WAJUMBE WAWILI ALIKUTANA NA NEEMA MARANGULA AKIWA NA MUME WAKE AMBAO WALIKUA WANAWAFUATA MAREHEMU NA BALOZI KWA AJILI YA KUZUNGUMZIA MZOZO WA NDANI YA NDOA YAO KWA HIYO WALIKUA WANAHITAJI KUSULUHISHWA, MAREHEMU NA WAJUMBE WAKE WAWILI WAKIWA PAMOJA NA BI NEEMA PAMOJA NA MUMEWE WAKIWA WANAJADILI TATIZO HILO HAPO BARABARANI MARA GHAFLA WAKATOKEA WATU WAWILI AMBAO WALIKUA WAKIPITA BARABARANI NA KUWAAMBIA MKO CHINI YA ULINZI NA MMOJA WAO AKATOA BUNDUKI NA KUMPIGA RISASI MAREHEMU AMBAYE ALIANGUKA CHINI HUKU WENZAKE WAKIKIMBIA KUJIOKOA KUTOKA ENEO HILO LAKINI PIA WALE WAHALIFU  WAKAKIMBIA NA KUTOKOMEA GIZANI VICHAKANI.
 
NDIPO WANANCHI WA ENEO HILO WALIJITOKEZA KWA MSAADA WA KUMSAIDIA MAREHEMU, WALIMCHUKUA MAREHEMU KUMKIMBIZA HOSPITALI KWA MATIBABU LAKINI ALIFARIKI DUNIA WAKIWA NJIANI. MAJERUHI BI NEEMA MARANGULA AMELAZWA HOSPITALI YA MKOA WA MWANZA SEKOU TOURE KWA MATIBABU NA HALI YAKE INAENDELEA VIZURI. MWILI WA MAREHEMU UPO HOSPITALI MKOA WA MWANZA SEKOU TOURE KWA AJILI YA UCHUNGUZI WA DAKTARI. CHANZO CHA MAUAJI HAYO BADO HAKIJAFAHAMIKA, UCHUNGUZI TUKIO HILO BADO UNAENDELEA.
 
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA JESHI LA POLISI AHMED MSANGI  ANAWAOMBA WANANCHI WENYE TAARIFA ZOZOTE KUHUSIANA NA TUKIO HILO ZITAKAZO SAIDIA KUFANIKISHA KUKAMATA WAHUSIKA WAZITOE  POLISI LAKINI PIA KUTOA USHIRIKIANO KWA VIONGOZI WAO NA KUHAKIKISHA WANATENGENEZA MAKAZI SALAMA HUKO WANAPOISHI NA MAENEO YA SHUGHULI ZAO. MSAKO MKALI UNAFANYIKA NA KUHAKIKISHA WAHUSIKA WA TUKIO HILO WANAKAMATWA.
 
IMETOLEWA NA:
SACP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages