Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
amesema kuwa, kusimama kidete, kutomfuata adui na kulinda utambulisho wa
kimapinduzi na Kiislamu ni sababu kuu za kuwa na nguvu mfumo wa
Kiislamu na taifa la Iran na kwamba, Marekani na madola mengine makubwa
yamekasirishwa mno na jambo hili.
Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema hayo katika hafla ya
kuapishwa na kupatiwa nishani wanachuo wahitimu wa mafunzo ya kijeshi
katika Chuo Kikuu cha Kijeshi la Imam Hussein AS na kusisitiza kwamba,
uistikbari umekasirishwa mno na hatua ya taifa la Iran ya kusimama
kidete na kuongeza kwamba, licha ya kambi ya uistikbari kutumia kila
wenzo na kufanya kila njama katika kipindi miaka 38 ili kuyasambaratisha
Mapinduzi ya Kiislamu lakini umeshindwa kufikia lengo lake hilo.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema, hii leo mabeberu
wanatumia kila wenzo, mashinikizo pamoja na njama za kiutamaduni,
kiuchumi, kisiasa, propaganda pamoja na vibaraka wao wasaliti ili
kuupigisha magoti mfumo wa Kiislamu hapa nchini na kuufanya ufuate
matakwa yao; lakini wameshindwa kufikia lengo hilo na lililowakasirisha
zaidi ni kuona taifa hili likiwa limesimama kidete na halitetereki na
wananchi wake hawako tayari kuufuata uistikabari.
Ayatullah Khamenei amesema kuwa, kuzusha makelele kuhusiana na
masuala kama ya nishati ya nyuklia, nguvu za makombora ya Iran na haki
za binadamu hapa nchini ni visingizio tu na kusisitiza kwamba, sababu
hasa ya uadui huu na huu uletaji visingizio ni hatua ya taifa hili ya
kukataa katakakata kuwa mfuasi wa uistikbari.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269