Serikali ya Libya imeuomba Umoja wa Ulaya uisaidie kulinda fukwe zake kupitia kutoa mafunzo kwa jeshi la majini la nchi hiyo.
Shirika la habari la Sputnik News la Russia limemnuukuu Bi
Federica Mogherini, Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya akisema
hayo na kuongeza kuwa, viongozi wa Libya wameuomba rasmi umoja huo uwape
mafunzo maafisa wake wa jeshi la majini kama njia ya kuisaidia kulinda
mipaka yake.
Mogherini amesisitiza kuwa, hatua hiyo ya viongozi wa Libya ni muhimu sana.
Ombi hilo la viongozi wa Libya lilitarajiwa kuwa moja ya ajenda za
kikao cha leo Jumatatu cha Baraza la Ulaya na ilitarajiwa kuwa, baada ya
kujadiliwa ombi hilo, kuchukuliwe hatua za lazima za kuwasaidia
wananchi wa Libya.
Siku ya Ijumaa pia, Mogherini alisema kuwa, Umoja wa Ulaya na jumuiya
ya kijeshi ya NATO zinaweza kuisaidia Libya kupitia kutoa mafunzo kwa
maafisa wake wa kijeshi wanaolinda fukwe za nchi hiyo kwa shabaha ya
kupambana na magendo ya silaha katika Bahari ya Mediterranean.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269