Mwezi Aprili mwaka huu umekuwa mwezi wenye
joto zaidi katika historia ya dunia, limesema Shirika la Hali ya Hewa
duniani WMO katika ripoti yake ya jana (Jumamosi).
Taarifa iliyotolewa la WMO inaonyesha kwamba wastani ya
halijoto ya mwezi Aprili imezidi wastani ya karne ya 20 kwa nyuzi 1.1 ya
Selisiasi.
Clare Nullis ni msemaji wa WMO na amesema, "joto tuliloshuhudia mwaka
2015 liligonga vichwa vya habari wakati ule, na tulikuwa na wasiwasi
mkubwa." Ameongeza kuwa Joto la mwaka 2016 linaifanya mwaka 2015
kuonekana afadhali.
Amesema sababu ya kwanza ya kuweko joto kubwa zaidi mwaka huu, ni
ongezeko la joto duniani na mabadiliko ya tabianchi yaliyosababishwa na
mikono ya binadamu.”
Kwa msingi huo Bi Nullis amesisitizia umuhimu wa kuchukua hatua mara
moja za kutekeleza makubaliano ya Paris ili kudhibiti mabadiliko ya
tabianchi.
Miji ya Afrika Mashariki kama vile Dar es Salaam, Mombasa na Nairobi
imekuwa ikishuhudia joto kali katika miezi ya hivi karibuni na hata
katika baadhi ya maeneo kusababisha vifo.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269