Maelfu ya raia wa Mali wamefanya maandamano
makubwa mjini Bamako, mji mkuu wa nchi hiyo kulalamikia utendaji duni wa
serikali na ufisadi mkubwa wa viongozi wa serikali.
Waandamanaji waliokuwa wamebebelea bendera zilizokuwa
zimeandikwa nara za kulaani ongezeko la kiwango cha juu cha ufisadi
nchini humo, wametaka kufanyika mabadiliko katika muundo wa kiuchumi na
kadhalika kuondoka madarakani Rais Ibrahim Boubacar Keïta wa nchi hiyo
ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 2013. Baadhi ya waandamanaji
walipiga nara zenye kauli kali dhidi ya serikali kutokana na miamala
mibaya inayofanywa na maafisa wa usalama na polisi ya nchi hiyo.
Kadhalika waandamanaji wametoa ripoti ya kutaka kukomeshwa ongezeko la
ufisadi wa kifedha na kiuchumi nchini humo, na kadhalika hatua zisizofaa
za serikali. Itakumbukwa kuwa, nchi ya Mali iliyo magharibi mwa
Afrika, ni moja ya nchi masikini zaidi duniani. Mbali na matatizo ya
kiuchumi, Mali inakabiliwa pia na ukosefu wa usalama unaosababishwa na
makundi ya wanamgambo wanaotaka kujitenga na nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269