Ikiwa ni siku moja baada ya Waziri wa Mambo
ya Ndani nchini Tanzania, Charles Kitwanga kupigwa kalamu nyekundu na
Rais John Pombe Magufuli kutokana na ulevi, wanasiasa na wasomi
mbalimbali nchini humo wameendelea kumbana zaidi wakisema hatua hiyo ya
rais imekuja ikiwa imechelewa.
Hayo ni baada ya wapinzani kumtaka Rais Magufuli kumuondoa
mapema kwenye nafasi hiyo kutokana na Kitwanga kuhusishwa na Kampuni ya
Infosys ambayo ilitoa ushauri kwa Kampuni ya Lugumi Enterprises
iliyopewa zabuni ya kufunga vifaa vya kuchukua alama za vidole (AFIS)
katika vituo vya polisi. Kwa upande wake, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
amesema uamuzi huo wa kutimuliwa Kitwanga ulikuwa sahihi na kwamba,
swali ambalo Kitwanga hakulijibu vizuri kutokana na hali ya ulevi,
litapaswa kujibiwa upya baada ya wabunge kuomba mwongozo wa swali hilo.
Waziri mkuu huyo ameongeza kuwa, Rais Magufuli ametengua uteuzi wa
waziri huyo Kitwanga kuanzia juzi. Wabunge wa chama tawala CCM na wale
wa upinzani wameitaja hatua hiyo ya rais wa Tanzania kuwa ilikuwa haki
kwa waziri kuachishwa kazi kwani alitia aibu serikali.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269