Mh. Charles Kitwanga aliekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema uamuzi wa Rais Dk. John Pombe Magufuli
kutengua uteuzi wa Waziri wa Mambo ya Ndani, Bw. Charles Kitwanga
umefuata kanuni za utumishi wa umma ambao unakataza mtumishi kulewa
akiwa kazini.
“Zipo
sheria za utumishi ambazo mtumishi hatakiwi kunywa pombe na wala hapaswi
kulewa akiwa kazini… mtumishi anapaswa kuwa na akili timamu
inayokuwezesha kufanya kazi za Serikali,” alisema.
Ametoa
ufafanuzi leo usiku (Ijumaa, Mei 20, 2016) wakati akijibu swali la
mwandishi wa TBC1aliyetaka kujua kama taarifa zilizoenea kuhusu
kutenguliwa kwa Waziri huyo ni za kweli.
“Ni kweli
Mheshimiwa Rais, Dk. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Waziri wa
Mambo ya Ndani, Mheshimiwa Charles Kitwanga kuanzia leo tarehe 20 Mei,
2016 baada ya kuonekana amelewa wakati wa kazi. Na hili lilibainika pale
alipokuwa akijibu maswali ya wizara yake leo asubuhi,” alisema Waziri
Mkuu.
Waziri
Mkuu amesema kuna swali aliloulizwa ambalo hakulijibu vizuri na kwamba
swali hilo litapaswa kurudiwa kuulizwa baada ya wabunge kuomba muongozo
wa swali hilo.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
DODOMA.
IJUMAA, MEI 20, 2016.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269