Michezo ya mwisho ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara,
inatarajiwa kufanyika kesho Jumapili, Mei 22, 2016 kwa timu zote 16
kutinga katika viwanja vinane tofauti kumaliza ngwe ya msimu wa 2015/16.
Michezo itakayopigwa kesho ni pamoja na Simba itakayokipiga
na JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati Azam FC ambayo
inawania nafasi ya pili kama Simba, itakipiga na African Sports kwenye
Uwanja wa Azam Complex, ulioko Chamazi, Mbagala nje kidogo ya jiji la
Dar es Salaam.
Mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yanga ya Dar
es Salaam inakaribishwa Majimaji ya Songea kwenye Uwanja wa Majimaji
mjini humo ilihali Mwadui na Kagera Stars zitamaliza ligi katika Uwanja
wa Kambarage mjini Shinyanga.
Kadhalika kwa mujibu wa ratiba hiyo ya Ligi Kuu ya Vodacom,
Toto Africans itakuwa mwenyeji kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini
Mwanza kuikaribisha Stand United, wakati African Sports ‘Wanakimanumanu’
wameifuata Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Manungu, Mvomero mkoani
Morogoro.
Mechi nyingine ya kukunja jamvi kwenye Ligi Kuu ya Vodacom
zitakuwa kati ya Mbeya City dhidi ya Ndanda FC ya Mtwara huku mchezo
mwingine wenye presha utakuwa ni kwa Tanzania Prisons yenye pointi 48
ambayo licha ya kucheza na Coastal Union ambayo tayari imeshuka daraja
kwenye Uwanja wa Mkwakwani, itakuwa inafukuziwa na Mtibwa Sugar kuwa na
nafasi ya nne. Mtibwa Sugar ina pointi 47 na mvutano ni wa nafasi ya nne
hasa ukirejea kwenye zawadi za Vodacom za Vodacom.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269