Mripuko wa homa ya manjano nchini Angola
umesababisha vifo vya watu zaidi ya 300 tangu mwezi Disemba mwaka jana,
huku kesi za ugonjwa huo zikienea hadi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo,
Kenya na hata Uchina.
Mripuko wa homa hiyo hatari uligunduliwa kwa mara ya kwanza
katika mji mkuu Luanda mwishoni mwa mwaka jana, na hivi sasa kesi za
homa hiyo zimeshathibitishwa kutokea katika mikoa mingi ya pwani na
katikati mwa Angola.
Shirika la Afya Duniani (WHO) lilisema jana katika ripoti yake kuwa,
Angola imeripoti jumla ya kesi 2,536 zinazoshukiwa za homa ya manjano
huku watu 301 wakiwa wameshaaga dunia hadi hivi sasa.
Taarifa ya WHO imeongeza kuwa, maambukizi ya virusi vya homa ya
manjano yangali yanachagiza katika baadhi ya wilaya, licha ya
kutekelezwa zoezi la utoaji chanjo katika miji ya Luanda, Huambo na
Benguela.
Shirika la Afya Duniani limeongeza kuwa, mripuko wa homa ya manjano
ungali unatia wasiwasi kutokana na kuendelea maambukizo katika mji mkuu
Luanda pamoja na kuwa hadi sasa watu zaidi ya milioni saba wameshapatiwa
chanjo.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269