Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri
ya Kiislamu ya Iran amelaani matamshi ya kuivunjia heshima Iran
yaliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia.
Sadeq Hussein Jaberi Ansari, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje
ya Iran leo amejibu matamshi ya uvunjaji heshima ya Adel al Jubeir
kuhusu uhusiano kati ya Iran na Iraq na kueleza kuwa, taifa la Iraq
halina haja na matamshi ya waziri wa Saudia ambayo katika kipindi cha
karibu muongo mmoja na nusu wa hivi karibuni imekuwa chanzo kikuu
machafuko na ugaidi huko Iraq, katika eneo la Mashariki ya Kati na
ulimwenguni kwa ujumla. Jaberi Ansari ameongeza kuwa, kuwepo washauri wa
kijeshi wa Iran huko Iraq chini ya uongozi wa Kamanda Qassim Suleimani
kumefanyika baada ya serikali ya Iraq kuiomba Jamhuri ya Kiislamu ya
Iran iitumie washauri wa kijeshi katika juhudi zake za kupambana na
magaidi na makundi yenye misimamo ya kufurutu ada, ambayo yamevuruga
amani na utulivu wa Iraq na eneo hili zima. Msemaji wa Wizara ya Mambo
ya Nje ya Iran amemtaka Adel al Jubeir asisahau kuwa nchi yake
inatambuliwa kimataifa kuwa ndiye muungaji mkono mkuu na hatari zaidi wa
ugaidi na kwamba ndiyo nchi inayosabaabisha kuenea machafuko duniani,
badala ya kujaribu kila awezalo kuzihadaa fikra za waliowengi na
kupotosha uhakika wa mambo. Adel al Jubeir Waziri wa Mambo ya Nje wa
Saudi Arabia jana alidai katika mahojiano na televisheni ya Russia al
Yaum kuwa eti Iran inaingilia masuala ya ndani ya Iraq.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269