Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (wa
pili kulia), akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi wa kukusanya
nguvu za pamoja kulinda haki za wasichana nchini Tanzania awamu ya pili
Dar es Salaam leo. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi kutoka Shirika la CDF,
Kashuma Mtengeti, Mwakilishi wa Shirika la Comic Relief Uk, DFID, Jane
Miller na Mwenyekiti wa Bodi ya Jukwaa la Utu wa Mtoto (CDF), Foturnata
Temu.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Mwakilishi
wa Shirika la Comic Relief Uk, DFID, Jane Miller, akizungumza katika
mkutano huo wakati akimkaribisha Wazir Ummy Mwalimu (kulia)
Mwenyekiti
wa Bodi ya Jukwaa la Utu wa Mtoto (CDF), Foturnata Temu (kulia),
akizungumza katika hafla hiyo wakati akitoa taarifa ya mradi huo.
Wadau mbalimbali na waandishi wa habari wakiwa kwenye hafla hiyo.
Mwakilishi kutoka Shirika la MBE FORWARD UK-Naana Otoo Oyortey akitoa mada kwenye hafla hiyo ya uzinduzi wa mradi huo.
Mwakilishi kutoka Shirika la CDF, Kambibi Kamugisha, akitoa mada.
Waziri Ummy Mwalimu akihutubia kabla ya kuzindua rasmi
mradi huo
Mwakilishi kutoka Wadada Centre, Christian Noah akitoa mada kwenye uzinduzi huo
Mkurugenzi kutoka Shirika la CDF, Kashuma Mtengeti, akichangia jambo.
Waandishi wa habari wakiwa kazini.
DK. Flora Myamba kutoka Repoa akitoa mada kwenye
uzinduzi huo.
Christine Mwanukuzi kutoka shirika la UNFPA, akichangia jambo.
Na Dotto Mwaibale
SERIKALI
imesema hata magereza zikijaa itaendelea kuwakamata na kuwachukulia
sheria kali wanaume wote wataka0 bainika kuwaoa au kuwapa mimba
wanafunzi.
Hayo
yalisema na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
wakati akizindua mradi wa kukusanya nguvu za pamoja kulinda haki za
wasichana nchini Tanzania awamu ya pili Dar es Salaam leo.
Mwalimu
alisema kuwa hata magereza yakijaa kwa kiasi gani serikali haitasita
kuwakamata watuhumiwa hao bila ya kuwaonea huruma bila ya kujali
mtuhumiwa ni mtu wa namna gani.
"Nawaagiza
maofisa Ustawi wa Jamii wote katika ngazi ya mikoa, wilaya na Kata
kuhakikisha haki za mtoto zinalindwa nchini kote hususan mtoto wa kike.
Ninataka wahakikishe wale wote wanao wapa watoto wa shule mimba na wanao
waozesha au kuoza wanakamatwa na kuchukuliwa hatua haraka kwani sheria
za kuwalinda watoto zipo, kinachotakiwa sasa ni utekelezaji" alisema
Mwalimu.
Waziri
Mwalimu alisema Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye kiwango cha juu cha
ndoa za utotoni ambapo taarifa ya Demografia na Afya ya mwaka 2010
zimeonesha kuwa kwa wastani wanawake 2 kati ya watano Tanzania wa umri
wa miaka 15-49 waliolewa kabla ya kufikisha umri wa miaka 18.
Aliongeza
kuwa utafiti wa hali ya afya ya uzazi, mtoto na malaria wa mwaka
2015/16 unaonesha kuwa idadi ya wasichana wanaopata watoto katika umri
wa miaka 15-19 imeongezeka kufikia asilimia 27 mwaka 2015 kutoka
asilimia 23 mwaka 2010 na kuwa tatizo hilo lipo zaidi katika mikoa ya
Katavi kwa asilimia 36.8, Tabora, asilimia 36.5, Simiyu asilimia 32.1,
Geita asilimia 31.6 na Shinyanga kwa asilimia 31.2.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Jukwaa la Utu wa Mtoto (CDF), Foturnata Temu alisema katika
kudumisha harakati za kupambana dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia
na mimba za utotoni vinavyoendelea kuwakumba wasichana nchini Tanzania,
CDF, Chama cha Uzazi na Malezi (Umati) na Kituo cha Wadada Centre
wameamua kuzindua mradi huo kwa pamoja ili kulinda haki za wasichana
hapa nchini.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269