Breaking News

Your Ad Spot

Sep 27, 2016

MAKONDA AKAGUA LEO MAANDALIZI YA KAMPENI YA UPANDAJI MITI ITAKAYOFANYIKA OKTOBA MOSI MWAKA HUU

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akijadili jambo na baadhi ya viongozi, alipokagua maandalizi ya kampeni ya upandaji miti itakayofanyika Oktoba Mosi mwaka huu, alipofika eneo la Gymkhana leo.  Wapili kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema na DAS wa ilaya hiyo, Edward Mpogolo.
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akitoa maelekezo kwa baadhi ya viongozi aliofuatana nao kukagua maadalizi katika eneo la Gymkhana, ya kampeni ya upandaji miti itakayofanyika Oktoba Mosi mwaka huu.
DAS wa wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo (kushoto) akitoa ushauri kwa Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (wapili kushoto) walipokagua maadalizi katika eneola Gymkhana, ya kampeni ya upandaji miti itakayofanyika Oktoba Mosi mwaka huu.
DAS wa wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo (kushoto) akitoa ushauri kwa Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (wapilikushoto) walipokagua maadalizi katika eneola Gymkhana ya kampeni ya upandaji miti itakayofanyika Oktoba Mosi mwaka huu.
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akijadili jambo na DAS wa wilaya ya Ilala Edward Mpogolo na Mkuu wa Wilaya hiyo Sophia Mjema, alipokagua maandalizi katika barabara ya Nyerere, ya kampeni ya upandaji itakayofanyika Oktoba Mosi mwaka huu,
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, PaulMakonda akijaribu bomba kati ya mabomba yanayotandazwa kwa njia ya kisasa kwa ajili ya kutumika kumwagilia maji, miti itakayopandwa eneo la Barabara ya Nyerere, wakati wa Kampeni ya upandaji miti utakaofanyika Oktoba Mosi mwaka huu
DAS wa wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo akinyoosha mkono kutoa ushauri wakati Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alipokagua katika eneo la Barabara ya Nyerere, maandalizi ya kampeni ya upandaji miti, itakayofanyika Oktoba Mosi mwaka huu.
Makonda na timu yake wakiendelea kukagua maandalizi hayo
Ukaguzi wa maandalizi hayo ukiendelea eneo la barabara ya Nyerere
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, akishuhudia uchorongaji wa ardhi kwa ajili ya kupitisha mabomba ya maji ya umwagiliaji miti, alipokagua maandalizi ya kampeni ya upandaji miti itakayofanyika Oktoba Mosi mwaka huu. Uchorongaji huo unaofanyika kitaalam unawezesha mabomba yanayotandazwa kupita chini ya barabara bila kuchimba barabara husika. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages