UMOJA wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi, UVCCM, taifa itatuma
mkaguzi wa hesabu na mali za jumuia hiyo
mkoa wa Arusha, katika kipindi cha wiki mbili kuanzia Septemba 27 mwaka huu ili
kupata ukweli zilipo shilingi milioni 112.8 za umoja huo zinazokusanywa kila
mwaka kutokana na kodi ya maduka.
Makamu mwenyekiti UVCCM, Taifa, Mboni Mhita, aliyasema hayo jana
mara baada ya kikao na wajumbe wa baraza la UVCCM ,mkoa wa Arusha,
kilichofanyika
ukumbi wa ccm ,mkoa na baada ya muda huo kamati ya taifa ya UVCCM,
itarejea
mkoani Arusha kufanyia kazi yaliyobainishwa na mkaguzi wa hesabu.
Mhita,ambae anaongoza kamati ndogo ya watu watatu ya UVCCM,taifa,alisema
anawashangaa wajumbe wa baraza hilo kushindwa kuchukua hatua na kusimamia
jumuia hiyo hadi washikane mashati wakati wao wakiwepo na sasa wanagombea
vibanda vya maduka ambavyo hawakuvijenga na wala hawajajenga vipya.
Mhita, alisema baadhi ya wajumbe wa baraza la UVCCM, Mkoa wa Arusha, hawaelewi maana ya UVCCM, majukumu yao kwa kuwa hawajasoma kanuni za umoja huo na wameingia kwenye uongozi bila kuwa na sifa na ndio chanzo cha migogoro.
Mhita, alisema baadhi ya wajumbe wa baraza la UVCCM, Mkoa wa Arusha, hawaelewi maana ya UVCCM, majukumu yao kwa kuwa hawajasoma kanuni za umoja huo na wameingia kwenye uongozi bila kuwa na sifa na ndio chanzo cha migogoro.
Wajumbe hao walikutana
na UVCCM kwenye mchakato wa kugombea
uongozi na hawajosoma kanuni na katiba
ya UVCCM hivyo kuwepo mitafaruku ndani ya umoja huo mkoani Arusha, ambayo
inakwamisha maendeleo na ufanisi wa
shughuli za umoja huo.
Alibanisha kuwa baraza lazima
libebe lawama kwa kushindwa kusimamia
majukumu kutokana na kushindwa kuendana na sera
za ccm kutokana na kukosa uadilifui, na kutokutambua majukumu yao.
Kamati hiyo ndogo inafuatilia mgogoro wa UVCCM ,mkoa wa
Arusha, ambapo miongoni mwa majukumu ya
kamati hiyo ni kuwasikiliza wajumbe wa baraza hilo kutokana na mgogoro
uliojitokeza hivi karibuni.
Mhita, alilitaja jukumu lingine la kamati hiyo ndogo kuwa ni
kupatiwa nyaraka za mikataba ya wapangaji wa maduka yote ya UVCCM, mkoa huo.
Aidha alisema kuwa baadhi ya
viongozi wa baraza hilo waliandika barua ya kuwatukana na kuwadharirisha
viongozi wa UVCCM taifa lakini leo walipoulizwa kwenye kikao hicho wamekana
saini zao.
Kwa upande wake Naibu katibu mkuu wa UVCCM taifa, Shaka Hamdu Shaka, alisema UVCCM ni taasisi kubwa ya Chama cha Mapinduzi hivyo lazima wazingatie heshima, umoja na ushirikiano kwa kuwa ndizo nguzo za uvccm.
Amewaambia kuwa UVCCM, Inaongozwa na kanuni, mbili za Utumishi na Utawala ,taratibu za fedha , maadili ya viongozi
Kwa upande wake Naibu katibu mkuu wa UVCCM taifa, Shaka Hamdu Shaka, alisema UVCCM ni taasisi kubwa ya Chama cha Mapinduzi hivyo lazima wazingatie heshima, umoja na ushirikiano kwa kuwa ndizo nguzo za uvccm.
Amewaambia kuwa UVCCM, Inaongozwa na kanuni, mbili za Utumishi na Utawala ,taratibu za fedha , maadili ya viongozi
Alisema kilichotokea kwenye uongozi wa UVCCM, mkoa wa Arusha
ni kutokufuatwa kwa kanuni ,taratibu na
miongozo ya jumuia hiyo.
Alibainisha kuwa ukiukwaji huo wa kanuni kumesababisha mgogoro wa
uongozi uliopelekea aliyekuwa mwenyekiti wake, Lengai kusimamishwa uongozi huku
aliyekuwa katibu wa mkoa Ezakiel Mollel, nae akiondolewa kutokana na kukaidi
maelekezo ya mwajiri wake kuhamia makao makuu.
Alisema kuwa anashangazwa kuona UVCCM ikiwa na wajumbe 16 wa
kamati ya miradi jambo ambalo ni kinyume na kanuni za UVCCM kwa kuwa hakuna
kifungu kinachoelekeza kamati iwe na wajumbe wengi kiasi hicho hata taifa haipo.
Aidha alisema UVCCM mkoa wa Arusha, inakusanya shilingi milioni
112.8 kwa mwaka makusanyo yanayotokana na maduka yaliyopo kwenye jengo la UVCCM
mkoa lakini hazijulikani ziliko.
Awali mjumbe wa kamati hiyo kutoka mkoa wa Lindi,Amir
Mohamed,aliwataka wanachama wa UVCCM mkoa wa Arusha, kujenga umoja
na,upendo na kuacha kushughulikiana wao
kwa wao na kusababisha migawanyiko ili kuiwezesha jumuia hiyo iweze kufikia malengo
na kutimiza majukumu yake ya kisiasa.
Mohamed, alikuwa akitoa salamu za UVCCM taifa, kwenye kikao
maalumu cha baraza la umoja wa Vijana mkoa wa arusha, iliyofanyika ukumbi wa
CCM, Mkoa kilichokuwa kikisikiliza mgogoro wa uongozi wa jumuia hiyo.
Alisema UVCCM ni tanuru la
kuoka viongozi na wajumbe wote wa
baraza hilo wana wajibu kufahamu
mipaka na misingi ya uongozi.
Alisema UVCCM,haitawavumilia watakaokiuka misingi na maadili itawatimua
hivyo lazima watumie rasimilami za umoja huo walinde zingine kwa manufaa kwa kuwa UVCCM ni walinzi wa mali za chama na viongozi wake.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269