Licha ya
chama cha CDU kuangushwa vibaya kwenye uchaguzi la kwao la
Mecklenburg-Vorpommern kutokana na sera yake ya wahamiaji, Kansela
Angela Merkel anasema sera yake ni sahihi na kamwe hatarudi nyuma.
Vichwa
vya habari katika magazeti na ripoti za televisheni na redio mara tu
baada ya CDU kushindwa uchaguzi huo wa Jumapili, zilitazamiwa kumrejesha
Kansela Merkel nyuma, na hotuba ya leo ilidhaniwa kuwa ingekuwa nyepesi
na laini. Lakini hivyo sivyo ilivyokuwa, kwani kwenye hotuba ya bungeni
ya leo Jumatano (7 Septemba 2016), ambapo alionekana kusimama imara.
"Hali
yetu leo ni bora zaidi kuliko ilivyokuwa mwaka mmoja uliopita kwetu
sote. Hapana shaka, bado kuna mambo ya kufanywa. Changamoto kubwa ikiwa
kuwarejesha nyumbani wahamiaji ambao hawawezi kubakia hapa na sisi. Na
kwa uadilifu kuwahudumia raia wetu, huku tukiwafahamisha kuwa tunapaswa
kuwasiaidia wale wenye haki ya kusaidiwa," aliwaambia wabunge.
Katika
hotuba hii, ambayo tayari imeshaonesha kuzua mjadala mkali, Kansela
Merkel amesema si kweli kuwa mmiminiko wa mamia kwa maelfu ya wakimbizi
nchini Ujerumani utapunguza mafao wanayopata raia wazawa wa Ujerumani,
hoja ambayo imekuwa ikitumiwa na wapinzani wake wa kisiasa.
Chama
chake, CDU, kiliangushwa kwenye uchaguzi wa mwishoni mwa wiki na chama
kinachopinga wahamiaji nchini Ujerumani, AfD, katika jimbo la
Mecklenburg-Vorpommern, kwa hoja hiyo hiyo dhidi ya wakimbizi.
Wapigakura
kwenye jimbo hilo walitumia nafasi hiyo kumuonesha kutokubaliana na
sera yake ya kufungua milango kwa wakimbizi na wahamiaji kutoka mataifa
yenye Waislamu wengi, hasa baada ya matukio kadhaa ya mashambulizi
kwenye miji ya kusini mwa Ujerumani, lakini kwenye hotuba yake ya leo
bungeni, Kansela Merkel amesema ugaidi si jambo linalohusiana moja kwa
moja na wakimbizi.
"Licha ya
kuwa tulikumbwa na mashambulizi mabaya ya Ansbach na Wurzburg, ugaidi
si jambo jipya lililokuja na wakimbizi kwetu. Hata kama si kila mkimbizi
anakuja na dhamira njema, hatupaswi kuwahukumu kijumla-jamala.
Kuifanya Ujerumani kuwa salama, ni pamoja na kuwaonesha wengine kwamba wanaadamu wenzetu wanaweza kututegemea sisi wanapokuwa na matatizo," alisema Kansela Merkel.
Kuifanya Ujerumani kuwa salama, ni pamoja na kuwaonesha wengine kwamba wanaadamu wenzetu wanaweza kututegemea sisi wanapokuwa na matatizo," alisema Kansela Merkel.
Makubaliano na Uturuki ni sahihi Sambamba
na hilo, alitetea pia namna anavyoliendea suala la mahusiano kati ya
nchi yake na Uturuki, akiwakosoa wale wanaomwambia ameshinda kulaani
hatua kali za ukandamizaji zinazochukuliwa na utawala wa Rais Tayyip
Erdogan baada ya jaribio la mapinduzi yaliyoshindwa mwezi Julai.
Merkel
amesema makubaliano kati ya Umoja wa Ulaya na serikali ya Uturuki
yaliyolenga kuzuia mmimiko wa wahamiaji yalikuwa hatua muhimu na
inayoweza baadaye kuigizwa kama msingi wa makubaliano na mataifa
mengine.
Mdahalo
wa jioni ya leo kuhusiana na hotuba hii iliyoshadidia msimamo na
muelekeo wa Kansela Merkel kwa masuala ya wakimbizi, usalama, na sera
yake ya nje unatazamiwa kuwa mkali sana.
Tayari
msuguano ndani ya serikali yake ya muungano umeshadhihirika, huku
mshirika wake mkuu, chama cha SPD kikionekana kujipanga kumpiku.
Upinzani
mkali pia umo ndani ya chake mwenyewe cha CDU, huku chama ndugu cha CSU
kikiwa tangu mwanzoni mbali sana na sera ya wakimbizi ya Kansela
Merkel. DW
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269