Meneja
wa Kituo cha kufua umeme kinyerezi I, Mhandisi Lucas Busunge, akifungua
kikao cha ujirani mwema kati ya TANESCO, TPDC na viongozi wa jamii
inayozunguka Vituo vya kufua umeme wa Gesi vya Kineterezi jijini Dar es
Salaam Septemba 30, 2016.
Mkuu wa Kitengo cha Usalama, TANESCO Makao makuu, Misana Gamba
NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said
SHIRIKA
la Umeme nchini TANESCO na viongozi wa dini, vyombo vya dola na viongozi wa
Serikali za Mitaa sita inayozungu vituo vya kufua umeme wa Gesi asili vya
Kinyerezi jijini Dar es Salaam, wamekubaliana kuweka mikakati ya pamoja
kuhakikisha jamii inashiriki katika ulinzi wa miundombinu ya umeme.
Makubaliano
hayo yamefikiwa leo Septemba 30, 2016, kwenye kikao cha ujirani mwema kati ya
TANESCO, TPDC, viongozi wa dini, viongozi wa serikali za mitaa na vyombo vya
dola ili kujadili namna bora ya kulinda miundombinu ya umeme kwenye vituo
hivyo.
“Umeme
wa Gesi ni umeme salama kabisa, hata hivyo ni wajibu wetu kushirikiana pamoja
kuhakikisha miundombinu ya umeme huu wa Gesi inatunzwa na kulindwa,”, Meneja wa
Kituo cha Umeme Kinyerezi I, Mhandisi Lucas Busunge alianza kwa kusema wakati
akiwakaribisha wajumbe kwenye kikao hicho.
Tumeona
tuitane hapa leo ili tujadiliane pamoja namna bora ya kuhakikisha umeme huu
utokanao na Gesi ambao Serikali imeiingia gharama kubwa, miundombinu yake
inalindwa na nyinyi viongozi mnao wajibu mkubwa wa kuwafikishia ujumbe wananchi
wanaoishi maeneo yanayozunguka mitambo hii. Alisema Mhandisi Busunge.
Akitoa
mada juu ya Mambo yanayoweza kusababisha uharibifu wa miundombinu ya umeme wa
Gesi na hasara inayoweza kulikumba taifa na jamii kwa ujumla, Mkuu wa Usalama
wa TANESCO makao makuu, Misana Gamba alisema, “Lazima tutambue kuwa Serikali
imewekeza fedha nyingi katika ujenzi wa vituo hivi na fedha hizi ni za walipa
kodi wa Tanzania, kwa hivyo ni wajibu wetu sote na sio TANESCO pekee
kuhakikisha tunalinda miundombinu hii kwa manufaa ya sasa na vizazi vijavyo,”
alisema Gamba
Akifafanua
zaidi, Mkuu huyo wa usalama alibainisha mambo ambayo jamii inapaswa kuelewa kuwa
ni hatari dhidi ya miundombinu ya umeme ambayo ni pamoja na kuwasha moto,
kulima au kuchimba mchanga, mmomonyoko wa udongo, wezi wa vyuma, uvuvi haramu, kujenga,
kufanya biashara au kuendesha magari makubwa sehemu ambayo miundombinu hiyo ya
umeme wa Gesi inapita.
Mkuu
huyo wa usalama wa TANESCO alisema, hatari inayoweza kutokea endapo mambo hayo
yatafanywa ni pamoja na kurudisha nyuma jiyihada za Serikali katika kuwaletea
umeme wananchi, lakini pia hatari ya kulipuka kwa mitambo hiyo ambapo madhama
makubwa yanaweza kuwakumba wananchi.
Akichangia
kwenye mazungumzo hayo, Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Leila Muhaji, ambaye
ndiye alikuwa muendesha kikao, alisema, Shirika la Umeme Tanzania, TANESCO,
imekuwa ikitoa elimu kwa umma juu ya umuhimu wa kutunza miundombinu ya umeme
kwa faida ya Watanzania wote, na hatua ya kikao hicho ni mwendelezo wa utoaji
elimu na kuwataka viongozi hao kuwa mabalozi katika maeneo yao, kwenye nyumba
za ibada, ili kusudi wananchi wengi waelewe umuhimu wa kuunza miundombinu ya
umeme ambayo kimsingi ni mali ya Watanzania wote.
Naye
afisa mwandamizi wa usalama Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini, (TPDC),
Elias Muganda, alitahadharisha juu ya shughuli za kiuchumi kwenye eneo
linakopita bomba la Gesi na ksuema hiyo ni hatari. “Kwa sasa kuna mabomba
mawili yenye Gesi tayari, ambayo yako umbali wa mita 2 kwenda chini, yakipata
mgandamizo unaosababishwa na magari makubwa kupita juu yake inaweza kupelekea
leakge na kusababisha Gesi kuvuja na matokeo yake kila mtu anayajua ni moto.”
Alifafanua
Akatoalea
mfano wa mabomba yaitwayo Carthodic Protection, ambayo huzuia kutu, lakini
tayari kuna watu wanang’oa vyuma hivyo na hii inaweza kusababisha kutu na
mabomba kutoboka,alitahadharisha, Muganda.
Wakichangia
mazungumzo hayo, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kanga, Shamte Mlanzi Mkali,
alitoa wito kwa viongozi wenzake wa Mitaa, kila wanapokutana kwenye vikao, moja
ya ajenda ya kuzungumza ni pamoja na usalama wa mitambo ya Gesi.
Hata
hivyo viongozi wengi walionyesha umuhimu wa TANESCO kutoa ajira kwa vijana
waishio maeneo ya jirani na mradi ili waweze kuona manufaa ya moja kwa moja ya
ujio wa mradi huo.
Mambo
yaliyoazimiwa kwenye kikao hicho ni pamoja na ulinzi wa miundombinu ya Gesi iwe
ni moja ya ajenda za vikao vya Serikali za Mitaa, na iwe marufuku kwa mtu
kupita au kukatiza eneo la Mitambo bila ya kibali maalum, uwepo utaratibu wa
kuwaalika viongozi wa TANESCO/TPDC kwenye vikao vya Serikali za Mitaa kama
itahitajika.
Maazimio
mengine ya kikao hicho kilichomuhusisha pia Mkuu wa upelelezi wa Kituo cha Sitakishari-Ukonga,
SSP, Hassan Okello, ni pamoja na kampuni
za ulinzi kwenye eneo la mitambo zijulikane kwa viongozi wa Serikali za mitaa
yote inayozunguka eneo la mradi.
Mitaa
iliyoshiriki kwenye kikao hicho ni pamona na Mtaa wa Kanga, Kibaga, Kinyerezi,
Kichangani, na Kifura.
Mhandisi Busunge
Kaimu
Meneja Uhusiano wa TANESCO, Leila Muhaji (aliyesimama), akizungumzia
umuhimu wa viongozi wa mitaa kushirikiana na TANESCO katika kuelimisha
umma, kutunza miundombinu ya umeme
Afisa
Usalama wa TANESCO makao makuu, Fidelis Almasi, akielezea namna
viongozi wanavyoweza kushiriki katika kuelimisha wananchi umuhimu wa
kutunza miundombinu ya umeme na athari za zitokanazo na uharibifu wa
miundombinu hiyo kwa jamii na serikali
Mkuu
wa upelelezi, Kituo cha polisi Sitakishari-Ukonga, MrakibuMsaidizi wa
Polisi, (ASP), Hassan Okello, akiwatoa hofu viongzoi hao kuhusu kutunza
siri wanapotoa taarifa za wahalifu na uhalifu na kwamba yeye binafsi
yuko tayari siku zote kuhakikisha usalama kwenye eneo hilo unazingatiwa
Afisa
Usalama Mwandamizi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini, (TPDC),
Eliasi Muganda, amesema, mabomba mawili ya gesi tayari yana gesi na yako
umbali wa kina cha mita 2 kutoka uso wa ardji na hivyo hayahitaji
mgandamizo kutoka juu kwani ni hatari yanaeza kupata nyufa na kuvujisha
Gesi
Afisa
Elimu wa Kata ya Kinyerezi, Mwalimu Mercy Mtei, (kulia), yeye amesema,
atawashirikisha walimu na wanafunzi kueneza ujumbe kwenye jamii
Sheikh Juma Swaleh wa Msikiti wa Othman Bin-Afan wa Kinyerezi
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kichangani, Niyukuli Leonard (kulia)
Mchungaji Jacob Msami, akizungumza
Ustaadhi Ally akizungumza
Mchungaji Ariel Mungereja wa Kanisa la EAGT, Kinyerezi
Afisa
Usalama wa Kituo cha Kinyerezi I, Furaha Munisi, akifafanua mambo
mbalimbali ya kiusalama ambayo viongozi hao wanapaswa kuyachukua na
kuwaelimisha wananchi
Picha ya pamoja baada ya kikao
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269