Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI), Dar es
Salaam, kwa mara ya kwanza imefanya
upasuaji mkubwa kwa mafanikio makubwa wa kunyoosha mfupa wa mgongo wa mtoto
uliopinda (Kibiongo) kitaalamu (Scoliosis).
Upasuaji huo umefanyika
kwa kutumia technolojia ijulikanayo kama ‘Posterior Instrumentation and Fusion’
ambayo inahusisha uwekaji wa vyuma maalum kwenye mfupa wa mgongo uliopinda
katika sehemu ya juu na chini ya mfupa wa mgongo na kuufanya mgongo unyooke inavyotakiwa.
Taassisi ya MOI imefanikiwa
kufanya upasuaji huo kupitia madaktari
bingwa wa MOI walioko kwenye mafunzo ya ubobezi wa juu katika upasuaji wa
mifupa na mgongo kwa watoto kwa
kushirikiana na madaktari bingwa kutoka Marekani.
Aidha, Uanzishwaji wa
upasuaji huu umetokana na kuanzishwa kwa ushirikiano wa kimafunzo kati ya
Taasisi ya MOI na Chuo cha madaktari bingwa wa upasuaji cha Afrika Mashariki ,
Kati na Kusini ‘COSECSA’ na Madaktari bingwa kutoka Marekani.
Uanzishwaji wa upasuaji
huu wa kunyoosha migongo ya watoto iliyopinda (Scoliosis) unatarajiwa kuisaidia
serikali kupunguza rufaa za kuwapeleka wagonjwa nje ya nchi ambazo ni za
gharama kubwa. Ambapo gharama za kumtibu mtoto mmoja nje ya nchi ni zaidi ya dola
za kimarekani elfu 30 hadi 40.
Hivyo, Uongozi wa
Taasisi ya MOI unatoa wito kwa madaktari kwote nchini kuja kupata mafunzo hayo
hapa MOI, Pia wazazi wenye watoto wenye matatizo hayo wawalete hospitali ili
wafanyiwe uchunguzi na upasuaji
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269