Mchuuzi
wa mbogamboga akipita karibu na takataka zilizoachwa bila ya kuondolewa
jirani na kituo cha daladala cha Tabata Kimanga mwisho Manispaa ya
Ilala, jijini Dar es Salaam.
Takataka zikiwa kando ya barabara.
Mwendesha
bodaboda akizikwepa takataka zilizoachwa bila ya kuondolewa jirani na
stendi ya daladala ya Tabataaa Kimanga mwisho jijini Dar es Salaam.
Na Dotto Mwaibale
WANANCHI
wa Tabata Kimanga Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam wameomba
kuondolewa kwa takataka zilizotelekezwa katika maeneo mbalimbali na
mkandarasi aliyepewa tenda ya kuziondoa.
Akizungumza na mtandao wa www. habari za jamii.com Dar
es Salaam juzi mkazi wa eneo hilo, Mfaume Wakwetu alisema katika maeneo
mengi ya Tabata Kimanga kunatakataka nyingi zimerundikwa kando ya
barabara bila kuondolewa na wahusika.
"Takataka
nyingi zimerundikwa katika eneo la stendi ya mabasi hapa Tabata Kimanga
na kuwa kero kubwa kwa watumiaji wa stendi hiyo na wapita njia" alisema
Mfaume.
Aliongeza
kuwa takataka zilitolewa majumbani huwekwa katika madampo madogo
yaliyoanzishwa kandio ya barabara lakini mkandarasi aliyepewa tenda hiyo
hushindwa kufika kwa wakati kuziondoa hivyo kuwa kero kwao.
Aliongeza
kuwa kutokana na takataka hizo kuachwa kwa muda mrefu bila kuondolewa
husambaa hadi kwenye mifereji ya maji taka ambayouziba na kusababisha
maji kushindwa kupita na kutoa hahrufu kali na kusababisha mafuriko mvua
zinaponyesha.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269