Serikali ya Cuba imetangaza habari ya
kufariki dunia Fidel Alejandro Castro Ruz, rais wa zamani wa nchi hiyo
mapema leo asubuhi akiwa na umri wa miaka 90.
Fidel Castro mbali na kuongoza mapinduzi
nchini Cuba mwaka 1959 hadi 1976 alikuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo, huku
akishika nafasi ya urais tangu mwaka 1976 hadi mwaka 2008. Chama cha
Kikomonisti ambacho ni chama pekee nchini Cuba kupitia mfumo wa chama
kimoja, kilikuwa madarakani kuanzia mwaka 1965 hadi 2011 chini ya Castro mwenyewe.
Katika kipindi cha utawala wake, taifa la Cuba lilishuhudia ukuaji wa
viwanda na biashara. Aidha rais huyo wa zamani wa Cuba anafahamika kama
hasimu mkubwa wa Marekani ambaye kwa kipindi chote aliendesha mapambano
makali ya kisiasa dhidi ya Marekani na hivyo kujipatia umashuhuri
mkubwa duniani.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269