Mbunge wa
Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete, wa kushoto akiwa na Afisa Mtendaji
wa Shirika lisilo la kiserikali toka Nchini Omani linaloitwa
TUELEKEZANE PEPONI Bw.Nasr Al Jahdhamy wakati wa kukabidhi visima
vitatu kwa wananchi wa jimbo hilo.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani
Kikwete, wa pili kutoka kushoto anayemfatia ni Afisa Mtendaji Bw.Nasr
Al Jahdhamy mwakilishi kutoka Oman na Katibu wa Mbunge Bwana Swala na
Mzee Maokola wakati wa kukabidhi visima vitatu kwa wananchi wa jimbo
hilo.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani
Kikwete, akiongea na wananchi wa jimbo hilo akiwa na Afisa Mtendaji wa
Shirika lisilo la kiserikali toka Nchini Omani linaloitwa TUELEKEZANE
PEPONI Bw.Nasr Al Jahdhamy wakati wa kukabidhi visima vitatu kwa
wananchi wa jimbo hilo.
Mbunge wa
Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete, na Afisa Mtendaji wa Shirika
lisilo la kiserikali toka Nchini Omani linaloitwa TUELEKEZANE PEPONI
Bw.Nasr Al Jahdhamy wakati wa kukabidhi visima vitatu kwa wananchi wa
jimbo hilo wakiwa katika picha ya pamoja na na baadhi wa watoto jimbo
hilo .
Mbunge wa
Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete amekabidhiwa visima Vitatu vyenye
thamani ya Shilingi Milioni 48.5 toka kwa Shirika lisilo la kiserikali
toka Nchini Omani linaitwa kwa TUELEKEZANE PEPONI chini ya Afisa
Mtendaji wake Nasr Al Jahdhamy.
Akizungumza
wakati wa kukabidhi visima hivyo Mbunge huyo alisema kuwa , shida ya
maji ndani ya Halmashauri ya chalinze imekuwa kubwa na kueleza kuwa kazi
iliyofanyika kufanikisha ujenzi wa visima hivyo ni kubwa ili kusaidia
tatizo hilo kwa kipindi hiki wakati wakisubiri kukamilika kwa ujenzi wa
mradi wa kutoa maji mto wami.
“Nimeona
nifanye kazi ya kutengeneza visima ili kupunguza ukali wa uhaba wa maji
kwani matengenezo ya mradi wa wami bado yanaendelea kuchimbwa kwa visima
hivi si ishara kuwa ule mradi wa maji ambao tuliongea kuwa umekufa
mradi wa wami utakapokamilika tunataraji utawanufaisha wananchi wengi wa
jimbo letu.”alisema Ridhiwani
Aidha
visima hivyo vitatu vimekabidhiwa katika kijiji cha matipwili , shule
ya sekondari ya matipwili na kijiji cha Gongo ambavyo vinaendelea
kujengwa na vinataraji kukamilika mapema ndani ya wiki ijayo.
Naye
Bwana Naseer aliahidi kuendelea kumsaidia Mbunge kufikia malengo yake ya
kusaidia kutatua changamoto zinazokabili nyimbo hilo,na kuongeza kuwa
atasaidia kuchimba visima vingine kumi katika Halmashauri hiyo na
kusaidia michezo.(P.T)
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269