Nchini
Uganda, Mfalme wa Rwenzururu, Charles Mumbere, amekamatwa Jumapili hii
tarehe 27 Novemba na atapelekwa katika mji mkuu, Kampala. Msemaji wa
polisi anasema Mfalme huyo anashitakiwa kwa "uchochezi wa vurugu".
Kukamatwa huko
kumetokana na kutokea kwa wimbi jipya la ghasia zilizoibuka wiki hii
nchini Uganda, katika mkoa wa Rwenzori unaopakana na Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo.
Wakati wa
makabiliano dhidi ya vikosi vya usalama vya Uganda, hali ilikua tete
siku ya Jumamosi ambapo watu 55 waliuawa. Mvutano katika mkoa huo
ulitokana na uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi Februari mwaka huu.
"Watu
wengi walipoteza maisha katika makabiliano hayo. Polisi kumi na wanne
waliuawa na washambuliaji 41 waliangamizwa ", polisi imesema Jumapili
hii asubuhi katika mkutano na waandishi wa habari. Maafisa wengine wanne
na askari wawili walijeruhiwa.
Wakati
ambapo polisi na jeshi walikua wakipiga doria karibu na kasri ya Mfalme
wa Rwenzururu asubuhi ya Jumamosi Novemba 26, "walinzi wa Mifalme
walishambuliwa kikosi hicho,"amesema msemaji wa polisi, Felix Kaweesi.
Mashambulizi
mengine yalitokea katika mkoa huo na gari la polisi lilichomwa moto.
Kwa mujibu wa polisi, mashambulizi haya yalikuwa "yaliandaliwa vizuri"
na washambuliaji walikua na vifaa vya kutosha ikiwa ni pamoja na
'bunduki' na 'mabomu.'
Kama
hakuna uhusiano wowote ambao utathibitishwa moja kwa moja kuwa ni waasi
wa mashariki mwa DRC walioendesha mashambulizi haya, pengine litakua
kundi la waasi wa Uganda wa ADF. Polisi bado inashuku uwezekano wa
kuwepo kwa mawasiliano hasa kwa kubadilishana silaha.
Sababu ya
vurugu hizi mpya inaonekana kuwa ni ya kisiasa na inahusishwa na nia ya
kuunda eneo huru nchini Uganda, Jamhuri ya Yiira.RFI
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269