Breaking News

Your Ad Spot

Feb 23, 2017

HATIMAYE JESHI LA IRAQ LAKOMBOA UWANJA WA NDEGE WA MOSUL, DAESH WAKARIBIA KUSHINDWA RASMI

Sambamba na kuanza hatua ya pili ya operesheni za kuyasafisha maeneo ya magharibi mwa Mosul, kaskazini mwa Iraq, jeshi la nchi hiyo limefanikiwa kudhibiti uwanja wa ndege wa mji huo ambao ulikuwa ngome kuu ya magaidi wakufurishaji wa Daesh (ISIS.)
Taarifa iliyotolewa leo na jeshi la Iraq imesema kuwa, jeshi la nchi hiyo limetumia mashambulizi mapana ya kila upande katika kuukomboa uwanja huo wa ndege wa al-Ghazlani kusini magharibi mwa mji wa Mosul. Taarifa hiyo imesisitiza kuwa polisi wa federali na kikosi cha radiamali ya haraka ya jeshi la Iraq wamefanikiwa kusonga mbele na kuwaswaga wanachama wa genge hilo la kigaidi kutoka uwanjani hapo.
Askari wa Iraq akionyesha eneo lililokombolewa kutoka mikononi mwa magaidi wakufurishaji wa Daesh (ISIS)
Inaelezwa kuwa, awali magaidi hao walitumia zana mbalimbali za kijeshi ikiwemo ndege zisizokuwa na rubani kwa lengo la kulizuia kusonga mbele jeshi la Iraq, juhudi ambazo hata hivyo zimeishia kufeli. Habari zaidi zinaarifu kwamba mamia ya wakazi wa maeneo ya magharibi mwa Mosul wameziacha nyumba zao na kwenda maeneo mengine kwa ajili ya usalama.
Jeshi la Iraq likizidi kusonga mbele kuwasaka magaidi wa Kiwahabi wa Daesh
Televisheni rasmi ya Iraq imeonyesha askari wa serikali wakiwasili katika uwanja wa ndege wa al-Ghazlani. Kabla ya hapo Jenerali Shakir Judat, kamanda wa jeshi la polisi nchini Iraq alinukuliwa akisema kuwa jeshi la Iraq lilizishambulia ngome muhimu za genge la Daesh katika uwanja huo wa ndege na kulitia hasara kubwa kundi hilo la Daesh linaloungwa mkono na Marekani, Israel na Saudi Arabia.
Waziri Mkuu wa Iraq, Haider al-Abadi
Operesheni ya kulikomboa eneo la magharibi mwa Mosul kutoka katika makucha ya wanachama wa genge la kigaidi na Kiwahabi la Daesh (ISIS) zilianza Jumapili iliyopita kwa amri ya Waziri Mkuu wa Iraq, Haider al-Abadi. Hii ni katika hali ambayo mwezi uliopita pia jeshi la Iraq kwa kushirikiana na harakati ya wananchi ya Hashdu sh-Shaab lilifanikiwa kuyakomboa maeneo ya mashariki mwa mji huo wa Mosul na kuwafanya maelfu ya wakazi wa meneo hayo kurejea makwao.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages