Kamishna Jenerali wa Jeshi la Uhamiaji Dkt. Anna
Makakala (kulia) akisaini kitabu cha wageni alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi
la Zimamoto na Uokoaji mapema leo asubuhi (kushoto) ni Kamishna Jenerali wa
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye
Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye aliyekaa katikati
mbele akiwatambulisha Viongozi Waandamizi wa Jeshi hilo kwa Kamishna Jenerali
wa Jeshi la Uhamiaji Dkt. Anna Makakala na kumueleza ni jinsi gani Jeshi la
Zimamoto linavyoendesha shughuli zake.
Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye akimkabidhi zawadi
ya bendera ndogo ya mezani Kamishna Jenerali wa Jeshi la Uhamiaji Dkt. Anna
Makakala ikiwa ni ishara ya umoja, ushirikiano na ukumbusho juu ya ziara yake
alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi hilo jengo la ushirika – mnazi mmoja mapema
leo asubuhi.
Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye (kushoto) akiwa
kwenye picha ya pamoja na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Uhamiaji Dkt. Anna
Makakala (kulia) mapema leo asubuhi alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la
Zimamoto na Uokoaji.
Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye akiwa kwenye picha
ya pamoja na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Uhamiaji Dkt. Anna Makakala na
Viongozi Waandamizi wa Jeshi la Zimamoto mapema leo asubuhi.
(PICHA
NA FC GODFREY PETER)
Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye atembelewa na
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Uhamiaji Dkt. Anna Makakala lengo ni kujifunza na
kukuza mahusiano kati ya vyombo hivyo viwili vya Ulinzi na Usalama.
Katika
ziara hiyo Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye,
alitumia fursa hiyo kumpongeza kwa kuteuliwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi
la Uhamiaji na kumuahidi ushirikiano katika kulijenga Taifa.
Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Uhamiaji Dkt. Anna Makakala ametembelea Makao Makuu ya
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji yaliyopo jengo la ushirika - mnazi mmoja jijini Dar es salaam, mapema leo asubuhi na alipata fursa ya kujifunza jinsi gani Jeshi
hilo linavyoendesha shughuli zake pamoja na kuwa na mazungumzo ya kina na
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji pamoja na Viongozi Waandamizi
wa Jeshi hilo. “Nimejifunza mengi lakini pia nashukuru kwa kupata fursa ya
kutembelea na kuona ni jinsi gani tunaweza kushirikiana” alisema Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Uhamiaji Dkt Anna Makakala.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269