Zoezi
la upimaji wa Afya Bure kwa wakazi wa Jiji la Mwanza na maeneo jirani
linalofanyika kwa siku tangu kuanzia jana, linaendelea katika viwanja
vya Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo nyuma ya Soko Kuu la Sabasaba
Ilemela.
Mchungaji
wa kanisa hilo, Dkt.Daniel Moses Kulola (kulia) amebainisha kwamba jana
zaidi ya wananchi 150 walijitokeza kupima afya zao ambapo zaidi ya 70
walihudumiwa na kurejea nyumba.
Alisema
zoezi hilo limejikita kwenye uchunguzi wa afya ya uzazi, kisukari,
presha pamoja na uzito likiongozwa na wataalamu wa afya kutoka Canada
wanaosaidizana na wataalamu wazawa.
#BMGHabari
Umati wa akina mama waliojitokeza kwenye zoezi la upimaji afya bure katika viunga vya kanisa la EAGT Lumala Mpya
Zoezi la kuchukua taarifa likiendelea kwa umakini
Zoezi hilo la upimaji afya bure linafanyika kwa siku mbili kuanzia jana
Zoezi hilo la upimaji afya bure linafanyika kwa siku mbili kuanzia jana na linasimamiwa na wataalamu wa afya kutoka Canada
Zoezi hilo la upimaji afya bure linafanyika kwa siku mbili kuanzia jana
Kwa wale watakaobainika kuwa katika hali ya uchunguzi zaidi watasaidiwa kufikishwa kwenye hospitali za rufaa ili kuhudumiwa.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269