Uchaguzi wa rais Somalia kufanyika leo, wagombea 22 wanachuana
Uchaguzi wa rais nchini Somalia unafanyika leo ukiwashirikisha wagombea 22 baada ya kuakhirishwa mara kadhaa.
Uchaguzi huo wa Rais wa Somalia uliakhirishwa kwa sababu kadhaa
ikiwa ni pamoja na kuongezeka vitisho vya kundi la kigaidi la al Shabab
na wasiwasi wa usalama katika nchi hiyo ya Pembe ya Afrika.
Ripori zinasema, kwa kuzingatia hali hiyo pia wabunge 275 na maseneta
54 wa Somalia wanatazaniwa kupiga kura katika eneo maalumu lenye ulinzi
mkali katika uwanja wa ndege wa Mogadishu.
Ripoti zinasema, kuna uwezekano mkubwa kwamba, uchaguzi huo utaingia
duru ya pili kutokana na ukweli kwamba, ni vigumu kwa mgombea yeyote
kupata thuluthi mbili ya kura zinazohitajika katika duru yake ya kwanza.
Mchuano mkubwa zaidi unatazamiwa kushuhudiwa kati ya Rais wa sasa wa
Somalia, Hassan Sheikh Mohamud, Waziri wake Mkuu, Omar Abdirashid Ali
Sharmarke na rais wa zamani wa Somalia Sharif Sheikh Ahmed.
Maafisa wa eneo linalojitawala la Somaliland wametangza kuwa, eneo
hilo halitashiriki katika uchaguzi wa leo wa rais. Eneo hilo limekuwa
likifanya jitihada za kujitenga na Somalia lakini hadi sasa suala hilo
halijakubaliwa na jamii ya kimataifa.
Usalama umeimarishwa sana mjini Mogadishu na maeneo mengine ya nchi hiyo kwa ajili ya kudhamini usalama wa wapiga kura.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269