Mkurugenzi
Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, (kushoto),
akizungumza jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, Dkt. Charels
Kimei, wakati wa uzinduzi wa ushirikiano baina ya taasisi hizo mbili
ambapo CRDB sasa itawakopesha Wanachama wa PSPF kwenye maeneo ya elimu,
viwanja na pesa za kuanzia maisha kwa watumishi wa serikali. Uzinduzi
huo umefanyika Februari 27, 2017 makao makuu ya PSPF jijini Dar es
Salaam.
NA K-VIS BLOG
WANACHAMA wa mfuko wa pensheni wa PSPF sasa wataanza kupata mikopo yao kupitia benki ya CRDB mara baada ya kuzinduliwa kwa mpango huo baina ya taasisi hizo mbili jana jijini Dar es Salaam.
Akizungumza kwenye hafla ya utiaji saini mpango huo , Mkurugenzi Mkuu wa
PSPF, Bw Adam Mayingu , alisema kuwa mpango huo wa kutoa mikopo kwa
wanachama ulianza tangu Desemba 2014 kwa kupitia taasisi nyingine za
kifedha.
Alisema kuwa PSPF na benki ya CRDB wamekubaliana kushirikiana
katika kuendesha kwa pamoja huduma ya mikopo.Mikopo hiyo ni pamoja na
mkopo wa elimu(education loan scheme), mkopo wa kuanzia maisha( startup
life loan scheme) na mkopo wa viwanja(Nipo site na PSPF).
Alisema
kuwa kwa upande wa mkopo wa elimu , mwanachama anaweza kukopa kwa ajili
ya kujiendeleza kielimu katika ngazi yeyote ya elimu .Ngazi hiyo ni stashahada, shahada, shahada ya uzamili na hata mafunzo ya ufundi.
Kwa upande wa mkopo wa kuanzia maisha, alisema mwanachama aliyepata ajira kwa mara ya kwanza huwa na mahitaji yake muhimu na kwa kutambua hilo, PSPF kwa kushirikiana na CRDB wameanzisha mpango huu ambapo mwanachama anaruhusiwa kukopa mishahara yake ya miezi miwili ili awaeze kujipanga na maisha mapya ya ajira.
Kuhusu mkopo wa viwanja kwa wanachama, alisema kuwa huduma hii itawawezesha wanachama wa PSPF kukopa na kumiliki viwanja vya makazi ambavyo vinapataikana maeneo mbali mbali ya nchi.
“Lengo kubwa
hapa ni kuwawezesha wanachama wa PSPF kumiliki viwanja vya makazi
vilivyopimwa iii kuwaepusha dhdi ya ujenzi katika makazi holela, ambayo
yamekuwa na gharama kubwa kuliko makazi yaliyopangiliwa”,alisema.
Alifafanua kuwa lengo kubwa la kuanzisha mikopo hiyo ni kuhakikisha kila mtanzania anatimiza ndoto yake ikiwa ni katika masomo kupitia mkopo wa elimu , ndoto yake nyingine kupitia mkopo wa kuanzia maisha au mkopo wa viwanja.
Hadi kufikia tarehe 17 Mwezi huu idadi ya wanachama walionufaika na mikopo hiyo na idadi kwenye mabano ni Elimu (1,432)), mkopo wa kuanzia maisha ( 847), mkopo wa viwanja (58).
“Kwa
kushirikiana na benki ya CRDB ambayo ina mtandao mkubwa wa matawi hapa
nchini tunaamini watanzania wengi watanufaika na mikopo hii na kwa
kufanya hivyo tutakuwa tunatakeleza juhudi za serikali ya awamu ya tano
ya kuhakikisha watanzania wengi zaidi wananufaika na huduma mbali mbali
za Mifuko ya Hifadhi ya jamii”, alieleza.
Kw
a upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk Charles Kimei,
alisema azma yao ni kuhakikisha kuwa ushirikiano na wadau wanamkomboa
kiuchumi mwananchi hususan mwenye kipato cha chini kwa kumpatia mkopo wenye riba ya asilimia 14 tu kwa mwaka. Kuhusu marejesho alisema ni kuanzia mwaka mmoja hadi miaka mitano.
Ushirikiano wetu na PSPF bado
una muendeleo ulio mpana kwani kwa pamoja tunadhamiria hapo baadae
kuingiza sokono mikopo kwa ajili ya wastaafu ‘pensioners’.
Alisema
mpango huu wa utoaji wa mikopo kw wastaafu una lengo la kuleta faraja
na kuwasaidia wastaafu katika kukidhi mahitaji yao mbali mbali ya
kimaisha ikiwamo kulipia gharama za matibabu, ada za shule za watoto au
wajukuaa na kuendesha biashara ndogo ndogo zitakazosaidia kupunguza ukali wa maisha ya kila siku.
Dk Kimei alifafanua kuwa nia
yao ni kujenga mazingira mazuri kwa wastaafu walio wanachama wa PSPF
ili kustaafu kusiogopwe na kuonekana ni mwanzo wa kuanza kwa kipindi cha
maisha ya shida yasiyokuwa na matumaini.
“Tunataka
kujenga tabia ya kuwafanya wafanyakazi wanapopata barua za kustaafu
wasihuzunike kama ilivyozoeleka”,alidokezaAlisema kuwa mwanachama wa
PSPF anayetaka mkopo anatakiwa aende kwenye tawi lolote la benki ya CRDB
ililopo karibu naye ili kupata huduma.
Bw.
Mayingu akitoa hotuba yake kuelezea ushirikiano huo ambao lengo lake
kubwa ni kupanuan wigo wa huduma kwa Wanachama wa Mfuko huo
Dkt. Charles Kimei, akitoa hotuba yake kueleza jinsi benki yake ilivyofurahishwa na ushirikiano huo
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi, akitoa hotuba ya ukaribisho
Mkurugenzi
wa Mipango na Uwekezaji wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bw. Gabriel
Silayo, (katikati), na Msaidizi Mtendaji wa Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB,
Bw.Keneth Kasigila, wakimsikiliza Mkurugenzi wa Wateja wa Mashirika wa
CRDB, Bw.Goodluck Nkini, (kushoto), wakati wa hafla hiyo.
Bw. Mayingu, (kushoto) na Dkt. Kimei, wakibadilishana mawazo muda mfupi kabla ya kufanyika kwa uzinduzi huo
Viongozi wa juu wa PSPF, wakipiga makofi wakati wa hafla hiyo
Baadhi ya maafisa wa CRDB waliohudhuria hafla hiyo
Baadhi ya maafisa wa PSPF
Baloziwa PSPF, Mrisho Mpoto, (kushoto), akiongoza kuimba wimbo wa taifa
Mkurugenzi
Mtendaji wa CRDB, Dkt. Charles Kimei, (kushoto) na Balozi wa PSPF, Bw.
Mrisho Mpoto (katikati), wakimsikiliza Afisa Uhusiano Mwandamizi wa
PSPF, Bw. Abdul Njaidi kabla ya kuanza kwa hafla hiyo
Baadhi ya maafisa wa PSPF waliohudhuria hafla hiyo
Mkurugenzi wa Mipangona Uwekezaji wa PSPF, Bw. Gabriel Silayo, akitoa neno la shukrani mwishoni mwa hafla hiyo
Anna
Lukando wa kampuni ya Ardhi Plan Limited, yenye ushirikiano na PSPF,
akizungumzia jinsi wanachamawa Mfuko huo wanavyoweza kufaidika
naupatikanajiwa viwanja vilivyopimwa kisheria
Maafisa wa PSPF na CRDB wakifuatilia hafla hiyo
Maafisa wa CRDB |
Meneja
wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari, (PSS), wa Mfuko wa Pensehni wa PSPF,
Bi.Mwanjaa Sembe, (kulia), akimkabidhi kadi ya kujiunga na mpango huo,
mfanyakazi wa CRDB, Bi. Fausta Urassa
Afisa
Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi, (kulia), akimkabidhi
kadi ya kujiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari (PSS), mfanyakazi wa
CRDB, Bw.Alfred Kessy.
Balozi wa PSPF, Bw. Mrisho Mpoto, (kulia),akimkabidhi kadi ya kujiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari (PSS), mfanyakazi wa CRDB, Bi. Flora Munisi. |
Picha ya pamoja ya wanachama wapya wa PSPF na maafisa wa Mfuko huo akiwemo Balozi Mpoto.
|
Uzinduzi rasmi ukifanyika
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269