Watu wasipoungua 8 wakiwemo watoto sita
wameuawa shahidi katika hujuma ya hivi karibuni ya ndege za kivita za
Saudia katika maeneo mbali mbali nchini Yemen.
Kwa mujibu wa taarifa, siku ya Jumamosi ndege za kivita za
Saudia zilishambulia mji wa bandarini wa Mukha katika Bandari ya Sham
yapata kilomita 346 kusini mwa mji mkuu, Sana'a ambapo watoto watano
wameuawa shahidi.
Aidha mke na mume na mtoto wao wamepoteza maisha baada ya ndege za
kivita za Saudia kudondosha mabomu katika nyumba moja iliyo katika
kijiji cha Manjada katika mkoa wa Dhamar, kusini magharibi mwa Yemen.
Hali kadhalka jana jioni ndege za kivita za Saudia zililenga kituo
cha kijeshi cha Khalid katika Wilaya ya Mawza kaskazini magharibi mwa
mkoa wa Ta'izz.
Katika kulipiza kisasi jinai hizo za Saudia, wapiganaji wa Kamati za
Wananchi wamewapiga risasi na kuwaua wanajeshi wawili wa Saudi Arabia
katika eneo la mkoa Jizan.
Wakati huo huo Mkurugenzi wa Utalii Yemen Abdulrahman al-Na'mi
amesema jeshi la Saudia limehujumu na kuharibu zaidi ya maeneo 200 ya
kitalii nchini Yemen na kuisababishia nchi hiyo hasara ya dola bilioni
4.5 tokea Machi mwaka 2015 hadi sasa. Aidha amesema hujuma hiyo ya
Saudia Yemen imepeleke karibu watu 90,000 kupoteza ajira katika sekta ya
utalii.
Saudia, kwa kushirikiana na waitifaki wake, ilianzisha hujuma za kila
upande dhidi ya Yemen tarehe 26 Machi mwaka 2015 kwa lengo la
kumrejesha madarakani kibaraka wake Abdrabbuh Mansur Hadi rais wa zamani
wa Yemen ambaye alijiuzulu nafasi hiyo na kukimbilia Saudia.
Hata hivyo licha ya Riyadh kufanya mauaji na uharibifu mkubwa nchini Yemen, imeshindwa kufikia malengo yake haramu nchini humo.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269