Kiongozi
mwanaharakati aliyeshiriki sana kupigana dhidi ya utawala wa ubaguzi wa
rangi nchini Afrika Kusini Ahmed Kathrada amefariki dunia akiwa na umri
wa miaka 87, wakfu wake umetangaza.
Bw
Kathrada alifariki dunia akiwa katika hospitali moja mjini Johannesburg
"baada ya kuugua kwa muda mfupi, kufuatia upasuaji aliofanyiwa kwenye
ubongo wake".
Pamoja na
Nelson Mandela, Bw Kathrada alikuwa miongoni mwa wanaharakati wanane wa
African National Congress waliohukumiwa kufungwa jela maisha mwaka
1964.
Walipatikana na hatia ya kujaribu kupindua serikali ya ubaguzi wa rangi.
Bw Kathrada alikaa jela miaka 26, 18 kati ya miaka hiyo akiwa katika gereza hatari la Robben Island.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269