Breaking News

Your Ad Spot

Mar 8, 2017

RISASI 360 ZAKAMATWA NA WATUHUMIWA SITA KUFIKISHWA MAHAKAMANI-KIGOMA

 Na Magreth Magosso,Kigoma

 JUMLA ya Risasi 360 na wawindaji haramu sita Mkoa wa Kigoma watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili kwa kukutwa na silaha za moto 11 za aina mbalimbali ,ikiwemo Marker Four na G3 sanjari na vipande 17 vya nyama aina ya Tohe na vipande 10 vya Nungunungu huku wakijua ni kinyume cha sheria ya uwindaji. 

 Mbali na hilo waokota kuni kadhaa katika msitu wa Mwibuye kwenye kijiji cha Mganza, kata ya mganza wilaya ya Kasulu Machi  1 ,2017 saa 2.45 asubuhi wakiwa katika harakati za kuokota kuni msituni humo walibaini mfuko wa plastiki ambao ulihifadhiwa risasi 109 za silaha aina ya G3 uliokuwa umefichwa chini ya mti. 

 Akibainisha hayo juzi ofisini kwakwe mbele ya mwandishi wa blog ya ujijirahaa Mkoani kigoma Ujiji,  Kamanda wa Polisi, Ferdinand Mtui alieleza kuwa, uelewa wa wananchi juu ya kubaini viashiria vya wahalifu ni matunda ya kupatikana kwa silaha hizo sanjari na watuhumiwa wa matukio hayo. “ndugu mwandishi matukio haya saba ni ya wiki moja tangu uanze mwezi huu, ambapo silaha za moto mbalimbali zimekamatwa kama gobore 8, mark four 1, risasi 319, huku risasi 156 za silaha aina ya SMG/SAR/ RISASI 10 silaha ya G3 na Short gun sambamba na gololi 44 za gobore” alifafanua DCP Mtui. 

 Aliyataja majina ya watuhumiwa waliokutwa na tuhuma hizo ni pamoja na Josephat Kanumwa(45) Gerishoni Bilatata(36), Kisore William(31), Japhet Mkuyu(40) na Juma Ndiyunguye(35) huku wengine wakifanikiwa kutoroka katika matukio ya uwindaji haramu, ambapo watafikishwa Mahakamani hivi punde baada ya uchakataji wa upelelezi kukamilika.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages