Typical Africanity ni nini?
Ndugu zangu,
Profesa Ayite anasema; " Ni hali ya kiongozi wa Kiafrika kuhofia kuandaa mrithi kwa hofu ya kufunikwa kisiasa". - Prof Ayite.
Hivyo
basi, tunaona hapa, kuwa dhana ya balance of power inakosa maana. Na
hili ni tatizo kubwa linalozikumba nchi nyingi za Kiafrika. Si kwenye
uongozi wa nchi tu, hata kwenye uongozi wa vyama na taasisi.
Jana
nimemwona Mugabe kwenye BBC News akiongea na vijana kijijini
alikozaliwa Chinoyi. Kimsingi alikuwa anazungumza na vijana ambao wengi
wao mwaka 1980 wakati Zimbabwe inapata Uhuru ama walikuwa ndio
wanazaliwa au walikuwa hajawazaliwa.
Mugabe anasikika akiwaambia vijana;
" I am not leaving, I am not dying"
Mugame
kama Kiongozi alishaondoka zamani, kisiasa alishakufa zamani.
Anachofanya sasa ni kung'ang'ania kivuli chake. Inasikitisha.
Ona
Mandela, katika uhai wake , mbali ya yeye kustaafu Urais, ameshuhudia
Rais mmoja mstaafu kutoka Chama chake cha ANC. Mugabe hatarajii kuitwa '
Rais Mstaafu' maana atafia madarakani.
Kwamba tangu Aprili
mwaka 1980 unaongoza nchi bila kumshuhudia Rais mwingine akiongoza nchi
hiyo hiyo, nacho ni kipimo cha udhaifu wa uongozi.
Maana, kwa
Zimbabwe, kuna waliozaliwa na kumkuta Mugabe madarakani, nao wamepata
watoto, na watoto nao wamepata watoto na kumkukuta Mugabe madarakani.
Ni ukweli, Zimbabwe ya sasa, mbali ya Mugabe, haina Mzimbabwe mwingine yeyote mwenye uzoefu wa kuongoza dola.Typical Africanity!
Inasikitisha.
Maggid.
Iringa.
Your Ad Spot
Jul 30, 2017
Home
Unlabelled
JAMII: MUGABE A TYPICAL AFRICANITY
JAMII: MUGABE A TYPICAL AFRICANITY
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269