Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo
akizungumza na wananchi wa kijiji cha Rutala wilayani Ukerewe mkoani Mwanza juu
ya utunzaji wa miradi ya maji.
--------------------
UKEREWE, MWANZA
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo amewataka
wananchi wa wilaya ya Ukerewe kutunza miradi ya Maji kwa kuwa serikali inaigharamia
kwa fedha nyingi.
Jafo aliyasema hayo alipotembelea mradi mkubwa wa maji wa
Kazilamkanda ambao utahudumia vijiji vipatavyo 13 wilayani humo.
Amesema serikali inafanya jitihada za kuwatatulia wananchi wake
kero mbalimbali ikiwemo ya upatikanaji wa huduma ya maji, hivyo ni vyema
wakatunza miundombinu ya miradi hiyo ili iweze kudumu kwa muda mrefu.
Akikagua mradi huo, Jafo alimpongeza Mkandarasi aliye jenga
chanzo na tanki la kuhifadhia maji la lita 680,000 ambaye ni Lutare Make
Enginnering Ltd kwa kazi nzuri.
Amesisitiza kukamilishwa kwa usambazaji wa Maji katika vijiji
vyote 13 kabla ya Disemba 30 mwaka huu.
Naibu Waziri huyo amesisitiza kulazwa mabomba yaliyo na ubora
ili kuepusha kupasuka kwa mabomba endapo mabomba hayo yatakuwa hayana viwango
na kusababisha hasara kubwa kwa wananchi na halmashauri baada ya kukabidhiwa
mradi husika.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi
Selemani Jafo akipata taarifa kuhusu miradi ya maji wilayani Ukerewe.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi
Selemani Jafo akipata taarifa kuhusu miradi ya maji wilayani Ukerewe.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani
Jafo akifanya ukaguzi wa tenki la maji
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani
Jafo akifanya ukaguzi wa mashine za kusukumia maji.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269