Na Tiganya Vincent, RS-Tabora
SERIKALI ya Mkoa wa Tabora imesema itakamata mali za Kampuni zilizopewa jukumu la kusambaza
pembejeo kwa ajili ya wakulima wa pamba ambao watawasambashia hasara wakulima ambao
watawasambazia mbegu mbovu za pamba ambazo hazitaota na dawa ilisoua wadudu.
Kauli hiyo imetolewa hivi karibuni na Mkuu wa Mkoa wa Tabora
wakati wa ziara yake ya kuwaelimisha wakulima wa pamba katika Wilaya ya Uyui.
Alisema kuwa hawezi kukubali wakulima wapate hasara na yeye akiwa
kiongozi anayebeba dhamana ya kuhakikisha kuwa anatumia vyombo vyote vinavyomsaidia
na kumshauri katika kulinda maslahi ya umma wakiwemo wakulima wa pamba.
“Kampuni itakayo
sambaza mbegu ambazo hazioti na dawa ambazo haziui wadudu nitamkamata yeye na mali zake zote ikiwemo magari na kupiga
mahesabu ya hasara waliyopata wakulima na kisha nitamwaandikia invoice ili aweze
kulipa gharama ya hasara hiyo ndio nitamwachia yeye na mali zao” alisema
Mwanri.
Alisema kuwa hesabu hiyo itahusu kulipa fedha ambazo mkulima
angepata kutokana na kilo ambazo angezalisha katika eneo lake na kwa kuzingatia
bei ya ununuzi wa pamba wa wakati wa mauzo.
Kwa upande wa Meneja Mbegu kutoka Kampuni ya Usambazaji Mbegu
ya Quoton Tanzania Limited Phineas Chikaura alimwahakikishia Mkuu huyo wa Mkoa
kuwa aina ya mbegu ni salama na kuwaomba wakulima kutochimba mashimo marefu
wakati wa upandaji wa mbegu za pamba kwa sababu zao hilo halina nguvu za
kusukuma udongo kama yalivyo mazao mengine.
Alisema kuwa wakichimba mashimo marefu upo uwezekano wa mbegu
kushindwa kuotoa na kudai kuwa ni mbovu.
Chikaura aliongeza kuwa pia wakulima hawapaswi kuloweka mbegu
za pamba kabla ya kupanda bali wanapaswa kugonja mvua inyeshe ndio wapande.
Alisema kuwa kitendo cha kuloweka wakati mwingine usababisha
mbegu ishindwe kuotoa endapo mvua ikichelewa kunyesha katika eneo husika.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269