RAIS MAGUFULI NA RAIS MUSEVENI |
Rais Dk. John Magufuli leo Novemba 9, 2017 ameanza ziara rasmi ya Kiserikali ya siku tatu nchini Uganda kufuatia mwaliko wa Rais wa nchi hiyo Yoweri Kaguta Museveni.
taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu imesema Rais Magufuli aliyeongozana na Mkewe Mama Janeth Magufuli amepokewa na mwenyeji wake Rais Museni akiwa na mkewe janeth Musen, katika eneo la Mtukula ambako ni mpakani mwa Tanzania na Uganda.
Raarifa imesema katika mapokezi Rais Dk. Magufulili amepigiwa mizinga 21 na kukagua gwaride rasmi lililoandaliwa kwa heshima yake na Jeshi la Uganda.
"Wakiwa mpakani hapo Marais wote wawili walitarajiwa kufungua kituo cha pamoja cha huduma za mpakani (One Stop Border Post - OSBP) kilichojengwa kwa lengo la kurahisisha taratibu za kiforodha, uhamiaji na kuharakisha biashara kati ya nchini hizi mbili", imesema taarifa hiyo.
Baadaye leo, Marais wote wawili wataweka jiwe la msingi katika mradi wa bomba la mafuta ghafi la kuanzia Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga nchini Tanzania, sherehe hizi zitafanyika katika kijiji cha Luzinga, kilichopo katika Mkoa wa Rakai nchini Uganda.
Taarifa imesema, baada ya ufunguzi huo, Rais Magufuli na Rais Museveni watazungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara utakaofanyika katika Wilaya ya Kyotera nchini Uganda.
"Jioni ya leo Rais Magufuli atahudhuria dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa kwa heshima yake na mwenyeji wake Rais Museveni katika Mji wa Masaka", imemalizia taarifa hiyo.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269