Zoezi la kumfanyia mgonjwa
upasuaji wa kuzibua mishipa ya moyo kupitia mshipa wa damu wa mkono
(Catheterization) kwa kutumia mtambo wa Cathlab likiendelea.
(Picha
na JKCI)
|
Na Mwandishi wetu
Leo Novemba 16, 2017 jumla
ya wagonjwa 20 wamefanyiwa upasuaji wa kuzibua mishipa ya moyo kupitia mshipa wa damu wa mkono
(Catheterization) kwa kutumia mtambo wa Cathlab hii ikiwa ni mara ya kwanza kwa
upasuaji wa aina hiyo kufanyika hapa nchini.
Akiongea na Waandishi
wa Habari leo jijini Dar Salaam Daktari bingwa wa magonjwa ya Moyo kutoka
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Peter Kisenge alisema upasuaji huo
unafanyika katika kambi ya matibabu ya Moyo inayofanywa na Taasisi hiyo
kwa kushirikiana na madakatari kutoka Taasisi ya Kimataifa ya Kiislamu ya
Misaada (IIRO) ya nchini Saudi Arabia.
Dkt. Kisenge alisema
kuwa kambi hiyo inaenda sambamba na utoaji wa elimu na kubadilishana ujuzi wa
kazi kati ya wafanyakazi wa Taasisi hizo mbili ikiwemo aina mpya ya
upasuaji wanaoufanya kitu ambacho
kinawajengea uwezo zaidi. ”
“Faida ya upasuaji huu
ni kumwezesha mgonjwa kutoka chumba cha upasuaji akiwa anatembea na baada
ya masaa manne kama hali yake inaendelea vizuri anaweza kuruhusiwa.
“Tofauti na upasuaji wa
kutumia mshipa wa paja ambao tulikuwa tunaufanya, baada ya upasuaji mgonjwa ni
lazima akae Hospitali kwa zaidi ya masaa 24 ili kuangalia maendeleo ya afya
yake”, alisema Dkt. Kisenge.
Kwa upande wake
Daktari bingwa wa magonjwa ya Moyo kutoka Taasisi ya IIRO Ali Al Masoud
alisema kambi hiyo inaendelea vizuri kwani kwa siku wanatibu wagonjwa 10 na
baada ya matibabu afya zao zinaimarika tofauti na ilivyokuwa kabla ya
matibabu.
Dkt. Masoud aliongeza
kuwa wamekuja na utaalam mpya wa kuzibua mishipa ya moyo kupitia mshipa wa damu wa mkono ambapo
kabla ya hapo matibabu yaliyokuwa yanafanyika ni ya kutumia mshipa wa damu wa
kwenye paja.
Alifafanua, “Hivi sasa
tunafanya upasuaji wa Moyo wa bila kufungua kifua kitu ambacho wenzetu
hawa walikuwa wanakifanya. Sisi tumewaongeza utaalam mpya wa kutumia
mshipa ya mkononi badala ya mshipa
wa paja.
Naye Bader Alanezi ambaye ni Mtaalamu wa magonjwa ya
Moyo na mishipa ya damu kutoka IIRO alimalizia kwa kusema kuwa wamepata muda wa kujifunza vitu vingi na kupata uzoefu mpya
wa baadhi ya magonjwa na mambo ya kiteknolojia ambayo katika nchi yao
hakuna.
Jumla ya
wagonjwa 40 wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji katika kambi hiyo ya siku
tano ambayo imeanza tarehe 14 hadi tarehe 18 mwezi huu.
Madaktari Bingwa wa Magonjwa
ya Moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Peter Kisenge na mwenzake
wa Taasisi ya Kimataifa ya Kiislamu ya
Misaada (IIRO) ya nchini Saud Arabia Ali Al Masoud wakimfanyia mgonjwa
upasuaji wa kuzibua mishipa ya moyo kupitia mshipa wa damu wa mkono
(Catheterization) kwa kutumia mtambo wa Cathlab katika kambi ya matibabu ya
moyo inayoendelea kwenye Taasisi hiyo. Jumla ya wagonjwa 40 wanatarajiwa
kufanyiwa upasuaji katika kambi hiyo ya siku tano.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269