Breaking News

Your Ad Spot

Jan 21, 2018

UVCCM TEMEKE WAFANYA BARAZA KUU KWA KISHINDO, WACHAGUA WAJUMBE WA BARAZA LA UTELEKEZAJI NA KUTHBITISHA KATIBU WA HAMASA

Fadhili Famonga
NA BASHIR NKOROMO, TEMEKE
Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam, leo umefanya kwa kishindo kikao chake cha kwanza cha Baraza Kuu kikiwa na ajenda moja ya  uchaguzi wa wajumbe wawili wa Baraza la Utekelezaji na kumthibitisha Katibu wa Hamasa wa Jumuiya hiyo Wilayani Temeke.

"Ndugu wajumbe, kikao hiki ni rasmi na ni cha kwanza baada ya kuchaguzi uliopita, ajenda yetu ni moja tu, kuchagua wajumbe wawili wa Baraza la Utekelezaji ambao watatokana na wagombea watatu, na pia kumthibitisha Katibu wa Hamasa atakayekuwa amependekezwa baada ya kikao Viongozi wa Bbaraza letu la utekelezaji", alisema Katibu wa UVCCM Wilaya ya Temeke Jamal Khinji.


Tamko hilo lilifuatiwa na Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Temeke, Fadhili Famonga kufungua kikao hicho na kisha shughuli ya kufanya uchaguzi ilifuatia hatua baada ya hatua.


Katika Uchaguzi huo uliofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Temeke, wagombea Esta Mapunda na  Ramadhani Msangi waliibuka kidedea baada ya kumbwaga Salama Faraji Hamisi ambaye hakuwepo ukumbini wakati wa uchaguzi huo. Salama alipata kura 37, wakati Ester akipata 49 dhidi ya kura 48 alizopata Ramadhani.


Baada ya matokeo, Mwenyekiti wa UVCCM Temeke na Katibu wake waliungana na Ramdhani na Ester katika kikao kifupi cha Baraza la Utekelezaji na kuibuka na pendekezo la jina la Rashid Ngajua ambaye wajumbe walilithibisha kwa kishindo kuwa Katibu mpya wa Hamasa, kuchukua nafasi ya Kurutmumu Amir ambaye amemaliza muda wake.


Mapema, Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Temeke aliwataka wajumbe kila mmoja kutambua kuwa kama watachagua viongozi bora katika uchaguzi huo wakatawezesha UVCCM katika wilaya hiyo kuwa imara na yenye uwezo mkubwa wa kuisaidia CCM katika kutimiza malengo yake.


"Tafadhalini kati yenu asithubu kumchagua mgombea yeyote kwa sababu ya urafiki au mahusiano yoyote, bali amchague baada ya kuamini kuwa anao uwezo wa kutoa mchango kutimiza malengo ya kuwepo UVCCM na siyo vinginevyo" alisema Mwenyekiti huyo.



HABARI KATIKA PICHA
Baadhi ya wajumbe wakibadilishana mawazo ukumbini kabla ya kuanza kikao cha Baraza Kuu la umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) kilichofanyika katika ukumbi wa manispaa ya Temeke Wilayani humo, leo
Katibu wa Hamasa na Chipukizi  aliyemaliza muda wake, wa wilaya ya Temeke Kuruthumu Amiri akizungumza na kufanya utambulisho mwanzoni mwa kikao cha Baraza Kuu la UVCCM kilichofanyika katika Ukumbi wa Manispaa ya Temeke wilayani humo, leo.
Katibu wa UVCCM Wilaya ya Temeke Jamal Khimji akitoa mwongozo kabla ya kumwalika Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Temeke Ramadhani Famonga(wapili kushoto) kufungua kikao hicho. Kushoto ni Mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM Taifa, ambaye alialikwa. Kulia ni katibu wa Hamasa na Chipukizi aliyemaliza muda wake Kuruthumu Amir
Wajumbe kutoka Vyuo na Vyuo Vikuu wakisimama walipotambulishwa.
Mwenyekiti wa Chipukizi Kata ya Yombo Vituka Salama Jeremia (kushoto) akiwa na wajumbe wenzake ukumbini wakati wa kikao cha Baraza kuu la Umoja wa Vijana wa CCM Wiaya ya Temeke, kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Manispaa ya Temeke, leo
Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya Temeke Ramadhani Famonga akimkaribisha mgeni mwalikwa Mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM Taifa Gwantwa Mwakijungu (kushoto), kuzungumza katika kikao hicho cha Baraza Kuu la UVCCM Temeke kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Manispaa ya Temeke. 
Mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM taifa Gwantwa mwakijungu akizungumza kwenye kikao hicho
Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Temeke Ramadhani Famoga akimshukuru Mwakijungu kwa hotuba aliyotoa kwenye kikao hicho.
Famonga akimsindikiza Mwakijungu wakati akiondoka ukumbini baada ya hotuba yake.
Mwakijungu akizungumza na Diwani wa Kata ya Kijichi Eliasa Mtarawaje baada ya kukutana naye nje ya ukumbi wakati akiondoka. katikati yao ni Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Temeke ramadhani Famonga akiwasikiliza. Kushoto ni Katibu wa Hamasa na Chipukizi wilaya ya Temeke aliyemaliza muda wake Kuruthumu Amiri
Wajumbe wakiwa ukumbini katika Kikao cha Baraza Kuu la UVCCM wilaya ya Temeke kilichofanyika leo katika ukumbi wa Manispaa ya Temeke, leo
Wajumbe wakiwa ukumbini wakati wa kikao hicho
Wajumbe wakiwa ukumbini wakati wa kikao hicho
Katibu wa UVCCM Wilaya ya Temeke Jamal Khimji akisisitiza jambo wakati wa kikao hicho
Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Temeke, Ramadhani Famonga akizungumza wakati wa Kikao cha Baraza Kuu la UVCCM wilaya hiyo, kilichofanyika katika Ukumbi wa Manispaa ya Temeke, Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu wa hamasa na chipukizi aliyemaliza muda wake Kuruthumu Amir na Katibu wa wa UVCCM Temeke, Jamal Khimji
Mjumbe akiomba ufafanuzi wa jambo wakati wa Kikao hicho
Mjumbe akiomba ufafanuzi wa jambo katika kikao hicho
Diwani wa Kijichi Eliasa Mtarawanje akiomba radhi kuchelewa kuingia katika kikao hicho, akisema amechelewa kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wake.
Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Temeke Ramadhani Famonga akifafanua jambo kabla ya uchaguzi kuanza kufanyika katika kikao cha Baraza Kuu la Jumuiya hiyo. Kulia ni Khimji
Aliyekuwa Mgombea wa nafasi mbili za kuwa Mjumbe wa Baraza la Utekelezaji UVCM Wilaya ya Temeke, Esta Mapunda akisimama kuomba kura kwa wajumbe.
Aliyekuwa Mgombea wa nafasi mbili za kuwa Mjumbe wa Baraza la Utekelezaji UVCM Wilaya ya Temeke, Ramadhani Msangi akiomba kura kwa wajumbe.
Mjumbe akitoa ufafanuzi kuhusu Mgombea Salma Faraja kutokuwepo ukumbini. Alisema mgombea huyo yupo safarini Uarabuni.
katibu wa UVCCM Wilaya ya Temeke Khimji akitoa maelezo ya namna ya upigaji kura.
Mjumbe akipiga kura
Mjumbe akipiga kura
Wajumbe wakipiga kura
Wajumbe wakipiga kura
Mjumbe akipiga kura
Mjumbe Ndugu Mtarawanje akipiga kura
Mwenyekiti wa Chipukizi Kata ya Yombo Vituka Salama Jeremia (12), akipiga kura
Katibu wa UVCCM Temeke Ndugu Khimji akipiga kura
Wagombea wakisindikizwa na Khimji kupeleka sanduku lenye kura katika chumba cha kuzihesabu 
Mwenyekiti wa Chipukizi Kata ya Yombo Vituka Salama Jeremia akisalimiana na Diwani wa Kijichi Eliasa Mtarawanje wakati wajumbe wakisubiri matokeo
Mwenyekiti wa UVCCM Temeke Ramadhani Famonga akizungumza na Mwenyekiti wa Chipukizi Kata ya Yombo Vituka Salama Jeremia (12) wakati yakisubiriwa matokeo ya uchaguzi
Katibu wa UVCCM wilaya ya Temeke Ndugu Khimji akitazama matokeo ya uchaguzi kabla ya kuyatangaza 
Waliokuwa wagombea wa ujumbe wa Baraza la Utekelezaji UVCCM Temeke Ester Mapunda na Ramadhani Msangi wakipongezana baada ya wote kuibuka washindi katika uchaguzi wa nafasi hiyo, uliofanyika katika ukumbi wa manispaa ya Temeke, Dar es Salaam, leo
Wajumbe wakishangilia baada ya matoke kutangazwa
Wajumbe wakishangilia kwa nyimbo
Baadhi ya wajumbe wakifuatilia hali ya mambo ukumbini
Wajumbe ukumbini
Mjumbe akihamasisha wenzake ukumbini
Wajumbe wakibadilishana mawazo ukumbini
Wajumbe wakibadilishana mawazo ukumbini wakati wakisubiri matokeo
Ramadhani Msangi na Ester Mapunda wakiwa meza kuu baada ya kutangazwa kushinda Ujumbe wa baraza la Utekelezaji kwenye kikao hicho. Kulia ni katibu wa UVCCM Temeke Ndugu Khimji na Mwenyekiti wa UVCCM Temeke Ramadhani Famonga.
Mjumbe wa NEC UVCCM mkoa wa Dar es Salaam, Jumanne Msagati akihamasisha wajumbe wenzake ukumbini
Mwenyekiti wa UVCCM Temeke Ramadhani Famonga akionyesha furaha ya dhati kwa uchaguzi kwenda vizuri katika kikao cha Baraza Kuu la UVCCM Temeke kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Manispaa ya Temeke Dar es Salaam. Kushoto ni Mjumbe wa Baraza la Utekelezaji UVCCM Temeke Ester Mapunda na kulia ni Katibu wa UVCCM Temeke Jamal Khimji
Mwenyekiti wa UVCCM Temeke Ramadhani Famonga akionyesha furaha ya dhati kwa uchaguzi kwenda vizuri katika kikao cha Baraza Kuu la UVCCM Temeke kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Manispaa ya Temeke Dar es Salaam.
"Sasa uchaguzi tumemaliza salama kilichobaki sasa tunawaletea jina la tuliyempendekeza kuwa Katibu wa Hamasa na chipukizi, kama itawapendeza naomba mlipitishe jina lake" akisema Famonga
Hali ukumbini
Wajumbe wakishangilia ukumbini baada ya meza kuu kumtaja Rashid Ngajua (aliyesimama kushoto), kuwa ndiye waliyenpendekeza kuwa katibu wa Hamasa na chipikuzi UVCCM Wilaya ya Temeke
Wajumbe wakimpongeza rashid Ngajua kwa kikao kumpitsha kuwa Katibu wa Hamasa na Chipukizi UVCCM wilaya ya Temeke, katika kikao cha Baraza kuu la UVCCM Temeke kilichofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Temeke Dar es Salaam, leo
Mwenyekiti wa UVCCM Temeke ramadhani Famonga (kulia), akimkaribisha  Ngajua kuzungumza na wajumbe
Ngajua akiwashukuru wajumbe, na kuahidi kuchapa kazi kuhakikisha uwepo wa Umoja wa vijana wa CCM Temeke unaonekana ndani ya CCM inavyostahili
Ngajua akizidi kupongezwa wakati akiimba wimbo wa hamasa
Meza kuu nao wakasimama kumshangilia
Meza kuu wakishangilia
Wajumbe wakishangilia
Ngajua akitamba meza kuu wakati akiimbisha nyimbo za hamasa
sasa ikabaki muda wa Mwenyekiti kupigapicha na wajumbe mbalimbali ukumbini






PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages