NA ESTOM SANGA-MBEYA
Waziri
wa nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Mheshimiwa George Mkuchika amewatembelea Walengwa wa Mfuko wa Maendeleo
ya Jamii-TASAF katika halmashauri ya Jiji la Mbeya na kuwataka kuongeza
jitihada zaidi za kujitegemea kwa kutumia ruzuku wanayoipata kwa
kuanzisha miradi ya uzalishaji mali ili kukuza kipato chao.
Mheshimiwa
Mkuchika amesema jitihada za serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya
Jamii-TASAF za kuhamasisha wananchi kuuchukia umasikini haziwezi kuwa
endelevu ikiwa walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya masikini hawatatumia
fedha wanazozipata kubuni miradi ya uzalishaji mali.
“hiki
mnachokipata kutoka serikalini kupitia TASAF kiwe chachu ya kuanzisha
miradi ya uzalishaji mali ili hatimaye muweze kujitegemea” amesisitiza
Waziri Mkuchika.
Akiwa
katika eneo la Shule ya Sekondari ya Lupeta katika jiji la Mbeya ,
shule ambayo TASAF imejenga jengo la Utawala na Maabara,Waziri Mkuchika
ameeleza kuridhishwa na matokeo ya ujenzi wa majengo hayo na kupunguza
kero iliyokuwa inawakabili walimu na wanafunzi shuleni hapo.
Aidha
Mheshimiwa Mkuchika amekutana na vikundi vya uzalishaji mali
vilivyoanzishwa na Walengwa wa TASAF kwa kutumia ruzuku ya fedha kupitia
Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ambapo walengwa hao wamekuwa
wakikopeshana fedha zinazotokana na uzalishaji wa bidhaa zikiwemo
mikeka,na hivyo kuwaongezea uwezo wa kuhudumia kaya zao.
Hata
hivyo Waziri huyo ametoa maagizo kwa uongozi wa mkoa wa Mbeya
kuhakikisha kuwa watu wanaonufaika na fedha za ruzuku kutoka TASAF ni
wale wanaokidhi vigezo vya umasikini na kutaka fedha zilizolipwa kwa
watu wasiostahiki zirejeshwe mara moja.
“rejesheni
fedha za serikali ili ziwanufaishe walengwa wanaostahiki kupata ruzuku
hiyo kama ilivyokusudiwa na serikali” ameonya Waziri Mkuchika.Kwa
upande wake Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Bi. Mercy
Mandawa ameishukuru serikali kwa kuendelea kuusimamia kikamilifu Mfuko
wa Maendeleo ya Jamii TASAF ili uendelee kusaidia jitihada za
kuwaondolea wananchi kero ya umaskini.
Amesema
tangu kuanzishwa kwa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini ,kumekuwa na
mwitikio chanya kwa walengwa kutumia ruzuku hiyo kuboresha maisha yao
huku mkazo ukiwekwa katika kuboresha elimu,afya na lishe kwa watoto
wanaotoka kwenye kaya za walengwa huku akisisitiza juu ya matumizi
sahihi ya ruzuku inayotolewa kila baada ya miezi miwili.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.
George Mkuchika (aliyevaa suti nyeusi) akikagua bidhaa zilizotengenezwa
na Walengwa wa TASAFkatika mtgaa wa Inyala katika jiji la Mbeya kama
njia mojawapo ya kujiongezea kipato.
Waziri
Mkuchika (aliyevaa tai) akimsikiliza mmoja wa wanafunzi wa shule ya
sekondari ya Lupeta katika jiji la Mbeya alipotoa maelezo ya maabara
iliyojengwa na TASAF shuleni hapo.
Waziri
wa nchi ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
Mhe. George Mkuchika akikagua jengo la maabara lililojengwa na Mfuko wa
Maendeleo ya Jamii-TASAF katika shule ya Sekondari ya Lupeta katika
halmashauri ya jiji la Mbeya.
Picha
ya juu na chini zinawaonyesha wanafunzi wanaotoka katika kaya za
walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini katika Mtaa wa Inyala
katika jiji la Mbeya wakitoa ushuhuda kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mhe. George Mkuchika (watatu kutoka
kushoto) namna wanavyonufaika na ruzuku kutoka TASAF
Baadhi
ya Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini katika mtaa wa Inyala
katika jiji la Mbeya wakiimba nyimbo mbele ya Waziri George Mkuchika
kushukuru hatua ya serikali kupitia TASAF kubuni Mpango huo ambao
wamesema umeleta chachu ya maendeleo katika eneo hilo.
Waziri
Mkuchika na viongozi wa mkoa na wilaya ya Mbeya pamoja na TASAF
wakisikiliza risala ya walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya
Masikini katika Mtaa wa Inyala (hayupo pichani) wakati waziri huyo
alipokutana na walengwa wa Mpango huo kuona namna wanavyonufaika na
huduma za Mpango huo unaotekelezwa na Serikali kupitia TASAF.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269