Breaking News

Your Ad Spot

Dec 13, 2009

MATUKIO KATIKA PICHA

MKAZI wa Kawe, Dar es Salaam, Khadija Mussa, akitafuta wateja wa samaki kwa wateja waliopumzika kwenye Klab ya Kawe Beach, jana, baada ya kununua samaki hao kwa bei nafuu kwa wavuvi. Alikuwa akiwauza samaki hao kwa sh. 40,000 wote. (Picha na Bashir Nkoromo).

BAADA ya bomba kukatika siku kadhaa bila kufanyiwa matengenezo, katika eneo la Kilimahewam Kawe Dar es Salaam, sasa kumegeuka bwawa lisilo rasmi na kusababisha maji kuendelea kupotea. Pichani, mtoto akichota maji katika 'kisima' hicho, jana.

LICHA ya joto kali lililopo jijini Dar es Salaam, makondakta walio wengi huvaa nguo ngungi zikiwemo za ndani. Pichani, mmoja wa makondakta akiwa amevaa kwa mtindo huo, wakati akiwa kazinai katika daladala la Kawe-Kariakoo, leo

MFANYABIASHARA na Kada wa CCM, maarufu kwa jina la Zahor Matelephone (wa pili kushoto) akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Rufiji mkoa wa Pwani, Kassim Majaliwa, simu 100, jana katika haflailiyofanyika katikaOfisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, mtaa wa Lumumba, Dar es Salaam. Siku hizo ambazo ni kwa ajili ya shughuli za CCM na serikali wilayani humo, amezikabidhi kutimiza ahadi aliyotoa kwa Rais Jakaya Kikwete alipokuwa Rufiji ambapo alimpokea CCM kigogo wa CUF, Mohammed Salehe 'Afif' (kushoto) ambaye ni shemeji wa mfanyabiashara huyo.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages