Breaking News

Your Ad Spot

Jan 24, 2010

VODA YAZINDUA KAMPENI YA WADAU WAKE KUCHANGIA MAAFA



Kampeni hiyo inajulikana hi hivyo
MKURUGENZI Mkuu wa kampuni ya Vodacom Tanzania  Dietlof Mare akizungumza na Waandishi wa habari katiuka uzinduzi wa kampeni hiyo, kwenye Ofisi za Vodacom mtaa wa Ohio, Dar es Salaam, leo.  Kushoro ni Mkurugenzi Kitengo cha Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Meja Jenerali Mstaafu, Bakari Shaban na kuliani Mkurugenzi wa Voda Foundation Mwamvita Makamba.
 Mkurugenzi wa Voda Foundation, Mwamvita Makamba akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo.WAPIGAPICHA wa vyombo mbalimbali vya hapari wakipigapicha wakati wa hotuba za uzinduzi wakampeni hiyo.

STORY
KAMPUNI ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania imezindua kampeni kwa wateja wake kutoa michango kwa waliofikwa na maafa kwa njia ya kutuma ujumbe mfupi wa maneno (sms) katika simu za mkononi.
Akizindua kampeni hiyo jana mjini Dar es salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom, Dietlof Mare alisema kampeni hiyo ni kwa ajili ya waliokumbwa na maafa katika wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro na Kilosa mkoani Morogoro hivi karibuni.
Mare alisema ili kutoa mchango mteja wa Vodacom atatuma ujumbe wenye neno 'Maafa' kwenda namba 15599 ambao utagharimu sh. 250 pamoja na kodi ya ongezeko la thamani (VAT) na anaweza kutuma mara nyingi kandri anavyoweza.
"Kampeni hii ni muhimu sana katika kuyerejesha katika hali ya kawaida maisha ya Watanzania walioathiriwa na maafa katika wilaya za Same na Kilosa", alisema.
Aliongeza, "hii si mara ya kwanza kwetu kufanya hivi, miaka kadhaa iliyopita taifa letu lilikumbwa na uhaba wa chakula Vodacom Tanzania tulikuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kwamba Watanzania hawafi kwanjaa".
Mkurugenzi wa Kitengo cha maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Meja Jenerali (mstaafu) Bakari Shaban, akizungumza kwenye uzinduzi huo alisema, Vodacom imefanya jambo muhimu ambalo kampuni nyingine hapa nchini zinatakiwa kuiga.
Alisema, licha ya kwamba jukumu lakusaidia waathirika katika majanga mbalimbali yanapotoikea ni lake, lakini haiwezi kufanikiwa ipasavyo kama haitapewa ushirikiano na jamii.
Mkurugenzi huyo aliwataka wateja wa Vodacom kujitokeza kwa wingi kutoa michango yao kupitia utaratibu huo kwa kuwa michango hiyo ni muhimu na bado inahitajika.

mwisho

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages