Kiingilio cha VIP 40,000/
PAMBANO la marudiano baina ya watani wa jadi, Yanga na Simba linarindima Jumapili wiki hii, kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Pambano hilo ambalo ni la Ligi Kuu ya Voda Tanzania Bara, awali lilikuwa linapigiwa chabo kwamba lingepigwa katika Uwanja wa kisasa wa Taifa, lakini akitangaza uwanja itakakovurumishwa amechi hiyo, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka haa Bongo (TFF), Frederick Mwakalebela, amesema utakuwa uwanja wa Uhuru al maarufu 'hamba la Bibi' hii ikiwa ni kukwepa gharama za kumihimi uendeshaji wa mechi ya watani hao.
Kwa kujibu wa Mwakalebela uamuzi wa kukipiga katika shamba la Bibi umefanywa na Simba na Yanga wenyewe kwa maelezo kwamba wanapoumaniana katika Uwanja wa taifa huwa hawanufaiki kimapato kulingana na mtanange wenyewe.
"Hakika uwamuzi wa mechi hiyo kuchezwa uwanja wa Uhuru haukufanywa na TFF bali Yanga na Simba wenyewe baada ya kukaa na viongozi wa timu hizo", alisema Mwakalebela kulinawaa soo ambalo lingetokea kwa baadhi ya mashabiki kudhani ni TFF iliyoamua mechi kutopigwa uwanja waupendao wa Taifa.
Kuhusu viingilio Mwakalebela amesema kiingilio cha juu (VIP) kitakuwa wekundu wanne (sh. 40,000) huku cha chinikabisa kikiwa sh. 7,000 huku wale wazito kiasi, watalipa sh. 30,000 kwenye jukwaa kuu na sh. 20,000 jukwa la kijani.
YANGA
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269