Breaking News

Your Ad Spot

May 6, 2010

MICHUANO YA KILI CUP

HATUA YA MAANDALIZI YAIVA KITUO 'E' CHA IRINGA
Habari katika picha  MCHEZAJI wa timu ya Ruaha Stars ya mkoa wa Iringa, Athumani Iddi 'Chuji' akiumiliki mpira timu hiyo ilipokuwa katika mazoezi yake leo katika uwanja wa Samora mjini Iringa, kujinioa kwa ajili ya michuano ya Kili Taifa Cup, hatua ya makundi itakayoanza kutimua vumbi, Jumamosi katika vituo sita nchini kikiwemo hiki cha Iringa.  TIMU ya Ruaha Stars ya mkoa wa Iringa ikifanya mazoezi leo katika Uwanja wa Samora mkoani humo kwa ajili ya maanadalizi ya michuano ya Kili Taifa Cup hatua ya makundi. Kushoto ni Ahtumani Iddi 'Chuji akiumiliki mpira.KOCHA Mkuu wa timu ya Ruaha Stars, Fred Felix Minziro (kulia) na kocha msaidizi wa timu hiyo Mussa Mahundi, wakiandaa vifaa vya mazoezi kwa ajili ya timu hiyo leo katika uwanja wa samora mkoani humo.WAPENZI wa soka wakishuhudia mazoezi ya timu  hiyo katika uwanja wa Samora
Story
MICHUNANO ya Kili Taifa Cup katika hatua ya makundi, inaaza kutimua vumbi Jumamosi hii katika vituo vyot sita huku maandalizi hatika kituo ‘E’.cha mkoa wa Iringa akielezwa kukamilika.

Msimamizi wa kituo cha Iringa, Eliudi Mvera alisema Pinda Boys kutoka mkoa wa Rukwa na Mapinduzi Stars ya Mbeya ndizo zitafungua dimba kwa kupepetana katika mechi itakayoanza saa 8 mchana na baada ya mechi hiyo timzu ya mkoa wa Kinondoni itajitupa kilingeni na wenyeji katika kituo hicho, Ruaha Stars ya Iringa.

Alisema, timu timu zitakazomenyana katika kituo chake, zilimeshawasili tangu jana.

Kulingana na ratiba iliyotolewa na Shirikisho la Soka nchini TFF, Jumapili itakuwa mapumziko na Jumatatu ndiyo Mbeya na Iringa zitaanza kuvaana na baadaye siku hiyo kumalizwa kwa kupambana timu za Kinondoni na Rukwa.

Jumanne pia ni mapumziko

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages