ops! Kiatu chamvuka Mama Clinton Ikulu ya Paris
Jan 31, 2010
NMB YATOA MSAADA SHULE YA MSINGI NYANZA, GEITA



JERRY MURO MATATANI KWA RUSHWA DAR?

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova anatarajiwa kutoa taarifa za undani wa tukio hilo, Blog hii inafuatili kupasha kadri taarifa zitakavyopatikana.
ZIARA YA WAZIRI MKUU MWANZA
MAHAFALI YA PILI CHUO CHA KODI
Jan 30, 2010
MKE WA WAZIRI WA AFRIKA KUSINI AKAMATWA
Sheryl Cwele (pichani), mke wa waziri wa masuala ya kijasusi wa Afrika Kusini amekamatwa kwa madai ya kuhusika na biashara ya dawa za kulevya.
Sheryl Cwele, mwenye umri wa miaka 50, mke wa Siyabonga Cwele, amefikishwa mahakamani akishtakiwa kwa jaribio la kuingiza cocaine nchini Afrika Kusini.Bi Cwele ameshtakiwa kwa kumtumia mwanamke mmoja kuchukua dawa hizo Uturuki na kumwajiri mwanamke mwengine kuzichukua kutoka Brazil.
Amewekwa rumande mpaka dhamana yake itakaposikilizwa katika wiki moja ijayo.
Bi Cwele anakabiliwa na shutuma hizo pamoja na Frank Nabolis, raia wa Nigeria aliyekamatwa Afrika Kusini mwezi Desemba.
VIONGOZI WA UENEZI WA CCM WILAYA NA MATAWI ILALA WATEMBELEA UPL
MHARIRI Mtendaji wa Kampuni ya Uhuru Publications Ltd, wachapishaji wa magazetiu ya Uhuru, Mzalendo na Burudani, Josiah Mufungo akimkaribisha katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM wilaya ya Ilala, Saidi Sidem alipowasili na makatibu wa siasa na uenezi wa kata za wilaya hiyo kufahamu shughuli mbalimbali za uzalishaji za UPL leo. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM tawi la UPL, Lucas Kisasa.
KIBASILA SEC KWAWAKA MOTOLEO BAADA YA MMOJA KUGONGWA NA GARI
Jan 29, 2010
STORY
ZAIDI ya Wanafunzi 20 wa shule ya sekondari, Kibasila, Dar es Salaam, wameumia hadi baadhi ya kupoteza fahamu katika ya vurugu zilizotokea jana baada ya mwenzao kugongwa na gari katika barabara ya Chang'ombe. Wanafunzi hao waliumia na baadhi yao kupoteza fahamu wakati Polisi wa kutuliza ghasia (FFU) walipokabiliana na wanafunzi wa shule hiyo kuwataywanya baada ya kufunga barabara huku wakirusha mawe kwenye barabara ya Chang'ombe.Walioshuhudia walisema, vurugu hizo zilitokea saa 4 asubuhi, baada ya mwanafunzi wa kidato cha sita katika shule hiyo Emmanuel Mapande kugongwa na gari katika barabara ya Chan'ombe, hatua chache kutoka makutano ya barabara hiyo na Mandela.
Mwalimi wa shule, Agnes Charles wa shule hiyo, alisema, Mapande alipelekwa katika hospitali ya Temeke ambako alipatiwa matibabu na hali yake ilikuwa inaenmdelea vizuri.
Alisema, baada ya mwenzao kugongwa wanafunzi walijawa na hasira na kufunga barabara kwa mawe huku wengine wakirusha mawe, hatua iliyofanya nagari kushindwa kupita eneo hilo kwa zaidi ya nusu saa.
"Ndipo baadaye walikuja FFU na kupiga mabomu ya machozi na kusababisha wanafunzi kukimbia hovyo hadi wengine kuumia na wengine kupotza fahamu", alisema mwalimu huyo.
Alisema, baadhi ya waliopoteza fahamu ni Agathha Kivunywa, Euster Hermitt, Fani Abdul, Kuruthum Athanas, Jacqueline Gades, Nary Richard, Janeth kagoa, Mary Shayo na Aneth Kiyogoma.
Wanafunzi hao walipelekwa hospitali ya Temeke, kwa kuchukuliwa shuleni hapo na gari la wagonjwa la hospitali hiyo ambalo liliitwa kuokoa maisha ya wanafunzi hao.
Wengine ambao walipekwa hospitali hawakuweza kufahamika mara moja kwa kuwa baadhi yao walaichukuliwas na walezi au wazazi wao waliofika shuleni hapo wakati wa vurugu.
Kamanda wa Polisi mkoa wa kipolisi wa Temeke, Reberatus Sabas hakupatikana kuzungumzia tukio hilo jana, kadhalika Kamanda wa polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Suleiman Kova hakulizungumzia.
"Tukio hilo linahusu mkoa wa Temeke, mtafute Kamanda Sabas atakueleza kwa kina", alisema Kova alipopigiwa simu na mwandishi wetu.
Wakizungumzia tukio hilo, baadhi ya wanafunzi walitaka sasa eneo hilo lamakutano ya barabara ya Chang'ombe na Mandela lililopokaribu na shule hiyo liwekwe taa za kuongoza magari.
Mwaka jana, ilipozuka tafrani eneo hilo baada ya amwanafunzi kugongwa, wanafunzi walidai yajengwe matuta hatua ambao ilitekelezwa, lakini licha ya kuwepo matuta ajali kamahiyo ya jana zimeendelea kutokea eneo hilo.
ciao.
ZIARA YA DK. SHENI KENYA
Jan 28, 2010
Picha zote na Mpigapicha wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Amour Nassor
TLTC YAKABIDHI MATREKTA YA SH.MILIONI 130 KWA VYAMA VYA TUMBAKU
MKUU wa Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya, Rashid Ndaile (katikati) akijaribu kuendesha moja ya matrekta manne yaliyonunuliwa na Kampuni ya Tumbaku Tanzania (TLTC) kwa ajili kuvikopesha vyama vinne vya msingi vya tumbaku wilayani humo. Hafla hiyo ilifanyika katika kijiji cha Lupa. Kulia ni Mkurugenzi wa Sheria na Uhusiano wa TLTC, Richard Sinamtwa.
STORY
Kampuni ya Ununuzi wa Tumbaku nchini(TLTC) imechukua hatua nyingine ya kukuza ushirikiano baina yake na vyama vya msingi vya tumbaku wilayani Chunya mkoani Mbeya kwa kuvikabidhi matrekta manne yenye thamani ya zaidi ya milioni 130.Akizungumza katika hafla ya makabidhiano yaliyofanyika kijiji cha Lupa, wilayani humo, Mkurugenzi wa Uhusiano kampuni hiyo, Richard Sinamtwa alisema matrekta hayo yatachangia kukuza zao,hivyo kuongeza kasi ya mapambano dhidi ya umaskini.
Alisema kuwa kampuni yake itafanyanyakazi bega kwa bega na wakulima wa zao hilo katika kutimiza nguzo zote za Kilimo Kwanza ili kuyafikia mapinduzi ya kijani nchini kwa kuwawezesha wakulima kuachana na jembe la mkono sawa sawa na mpango wa kuendeleza kilimo bora nchini ASDP.
Sinamtwa alivitaja vyama vinavyonufaika na mpango wa matrekta hayo kuwa ni Majengo, Upendo, Kalangali na Nkung’ungu, ambapo alisema vyama hivyo vitarejesha chini ya nusu ya gharama ya ununuzi wa matrekta hayo katika muda maalum.
Alisema kampuni yake ikifanya kazi na washirika wake itaendelea kuvisaidia vyama vya msingi vya ushirika vya tumbaku kwa kuvipatia huduma za ughani na mbegu bora zinazolishwa katika mashamba yake ya mfano yaliyoko Urambo,mkoani Tabora, Likenangena mkoani Ruvuma na Lupa yenyewe.
Simtawa alisema pamoja na mradi huo wa matrekta, kampuni yake imeanzisha mpango umwagiliaji vitalu vya tumbaku pamoja na mazao ya chakula, ambapo tayari imegawa bure pampu 200 kwa wakulima hao.
Katika hotuba yake, Mgeni rasmi katika hafla hiyo,Mkuu wa Wilaya ya Chunya,Rashid Ndaile alisema matrekta hayo yamekuja sambamba na mkakati wa kitaifa wa 2025 wa kupunguza umaskini pamoja na kilimo Kwanza ambayo yote inahimiza matumizi ya zana bora za kilimo.
Alisema miikakati yote miwili ASDP na Kilimo Kwanza inahimiza matumizi ya zana bora za kilimo kunavyoweza kumletea tija bora mkulima,” alisema huku akiwapongeza TLTC ambao kama sekta binafsi wameonesha njia kwa kuwasaidia wakulima na serikali katika kufikia malengo yake ya maendeleo.
Ndaile aliwaasa wakulima hao kutumia vyema pesa zinazotokana na tumbaku kwa kuhifadhi akiba ya chakula,kusomesha watototo shule, kujenga nyumba bora pamoja na kuwekeza katika miradi ya maendeleo.
Akizungumza kwa niaba ya wakulima wenzake, Alex Mtalisi kutoka chama cha msingi cha Kalangali aliwashukuru TLTC,akisema misaada inayotolewa kwao siku kwa siku itazidi kulikuza zao la tumbaku nchini.
Aliiomba TLTC izidi kuwasaidia hususani katika ujenzi wa mabanda yanayotumia kuni kidogo wakati wa ukaushaji wa tumbaku.
JENERALI SARATH FONSEKA APINGA MATOKEO YA UCHAGUZI

CHAMELEON ANATAFUTWA NA POLISI?
kusoma habari ya udaku ambayo ilimkera.

story
Wateja wa Zain Tanzania nchi nzima sasa watarudishiwa papo kwa papo pesa yoyote watakayotumia kuzungumza kwenye simu zao zao mkononi kupitia ofa kabambe ya Nipe Nikupe.
Zain, kampuni inayoheshimika zaidi nchini Tanzania imethibitisha leo kwamba mteja wa Zain atarudishiwa shilingi 200 papo kwa papo kwa kila shilingi 200 atakayotumia kuzungumza kila siku. Hii inamaanisha kwamba kila shilingi 200 inayotumika kuzungumza kwenye mtandao wa Zain inakurudishia kiashi hicho hicho ili uweze kuendelea kuzungumza kwenye mtandao wa Zain inamrudishia mteja akitumia shilingi 200 kwenye simu ya kutoka mtandao wa Zain kwenda Zain atarudishiwa kiasi hicho cha pesa ili akitumie kwenye mtandao mwingine
Ofa ya Nipe Nikupe itaendelea kutoa fursa kwa wateja wa Zain wanaohitaji kuwasiliana na ndugu na familia au kufanikisha mahitaji yao ya biashara nchini kote kunufaika na mtandao mpana wa Zain ulioenea maeneo mengi zaidi nchi kuliko mtandao mwingine wowote pamoja na bidhaa za ubunifu wa hali ya juu. Wateja wa Zain wataweza kutumia bonasi walizopata kupiga simu kwenda Zain au mtandao mwingine wowote siku hiyo hiyo kabla muda wa bonsai haujaisha saa sita usiku.
Kujisajili katika Nipe Nikupe mteja wa Zain anapaswa kutuma SMS ya neno NIPE mara moja tu kwenda 15444 na ujumbe huo utagharimu Tshs 500 tu ambayo itatozwa mara moja tu.
ALIYEZALIWA NA MIGUU NA MIKONOMINNE AANZA SHULE NDIA
Mtoto wa nchini India ambaye alizaliwa akiwa na miguu minne na mikono minne, ameanza shule miaka miwili baada ya kufanyiwa operesheni ya kuviondoa viungo vilivyozidi.
Lakshmi Tatma alichukua nafasi kubwa kwenye vyombo vya habari alipozaliwa katika mji wa Bihar nchini India miaka minne iliyopita akiwa na miguu minne na mikono minne.
Lakshmi alizaliwa mwili wake ukiwa umeungana kuanzia kiunoni na pacha mwenzake ambaye alikuwa hana kichwa na hivyo kumfanya awe na jumla ya miguu minne na mikono minne.
Wakati huo kutokana na maumbile yake ya ajabu Lakshmi alikuwa akiabudiwa kama mungu wa kihindu.
Mtoto Lakshmi Tatma kabla ya oparesheni akiwa na mama yake.
Baada ya operesheni kubwa iliyofanyika miaka miwili iliyopita ambayo ilimalizika kwa mafanikio makubwa, miguu na mikono iliyozidi kwenye kiwiliwili chake iliondolewa.
Hivi sasa Lakshmi ametimiza miaka minne na ameanza shule sambamba na watoto wenzake.
"Nikifikiria jinsi alivyokuwa, sikutegemea Lakshmi angeweza kwenda shule au angekuwa na maisha aliyo nayo sasa", alisema mama yake Poonam, mwenye umri wa miaka 26.
"Vitu vyote ambavyo anaweza kuvifanya sasa alikuwa hawezi kuvifanya kabla ya operesheni, alikuwa hawezi hata kukaa lakini sasa anaweza hata kukimbia na kucheza na watoto wenzake", aliendelea kusema mama yake.
Lakshmi pamoja na kwamba hivi sasa amepona kabisa bado anahitajika kufanyiwa operesheni zaidi baada jinsi anavyozidi kukua ili kuvirekebisha

Lakshmi akiwa na furaha pamoja na mama yake baada ya oparesheni.
MREMA AENDA INDIA KUTIBIWA
MWENYEKITI wa TLP, Augustine Mrema yuko nchini India kwa ajili ya matibabu ya ugonjwa wa kisukari. Mrema, ambaye aliondoka wiki iliyopita, atakuwa akitibiwa Hospitali ya Appollo iliyopo jijini Bambay. Kaimu katibu mkuu wa TLP, Hamad Tao alisema Mrema amekwenda India ili kukutana na wataalam wa ugonjwa huo."Amekwenda tangu wiki iliyopita na atakaa huko kwa wiki tatu ili wataalam waweze kumpatia matibabu,"alisema Tao.
Alisema kuwa huo umekuwa ni utaratibu wa Mrema, ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, kwenda India kutibiwa ugonjwa huo ambao umekuwa ukimsumbua kwa muda sasa na kwamba Mrema anagharimia mwenyewe matibabu yake na kwamba hatumii fedha za TLP.

Mweeyekiti wa TLP Augustine Mrema akimuombea kura kwa wananchi mgombea wake wa ubunge katika uchaguzi mdogo wa Biharamulo, Juni mwaka jana.
Alisema kuwa huo umekuwa ni utaratibu wa Mrema, ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, kwenda India kutibiwa ugonjwa huo ambao umekuwa ukimsumbua kwa muda sasa na kwamba Mrema anagharimia mwenyewe matibabu yake na kwamba hatumii fedha za TLP.
Mweeyekiti wa TLP Augustine Mrema akimuombea kura kwa wananchi mgombea wake wa ubunge katika uchaguzi mdogo wa Biharamulo, Juni mwaka jana.
MCHAPO
JAMAA alikwenda kununua sigara dukani, baada ya kupatiwa sigara jamaa akatoa kibiriti ili kuiwasha aanze kuivuta pale pale dukani.
Muuzaji: Tafadhali usivutie hapa sigara.
Jamaa: Kwanini, mbona umeniuzia wewe hapa hapa?
Muuzaji: Sawa, je? kama ningekuuzia katarasi ya chooni ungeitumia hapa hapa pia?
mdau wa Chachandu-Daily. Email: mgosius5@yahoo.com
Muuzaji: Tafadhali usivutie hapa sigara.
Jamaa: Kwanini, mbona umeniuzia wewe hapa hapa?
Muuzaji: Sawa, je? kama ningekuuzia katarasi ya chooni ungeitumia hapa hapa pia?
mdau wa Chachandu-Daily. Email: mgosius5@yahoo.com
LIGI KUU YA VODA; MAJIMAJI YATOSHANA NGUVU NA JKT RUVU
Jan 27, 2010
MWANA-BLOG WETU BASHIR NKOROMO NA VIJANA WAGENI WA KIJAPAN
WANAJESHI WANAODAIWA KUMUUA SWETU WATINGA KIZIMBANI
STORY KWA UFUPI......
WATU wawili wanaosemekana kuwa ni mtu na mkewe ambao ni wanajeshi wa Jeshi la Ulinzi la Weananchi wa Tanzania, mchana huu wametinga kizimbani katika mahakama ya Hakim Mkazi Kisutu dar es salaam, kwa tuhuma za kumua Swetu Fundikira kwa kipigo.
Washitakiwa hao MTM 1900 Sajenti Roda Robert (42) JKT, Mbweni na MT 75854 Koplo Ally Ngumbe (37) wa JWTZ Kunduchi, Dar es Salaam wamefikishwa mbele ya Hakimu Mkazi Geni Vitus Dudu na mashtaka yameendeshwa na wakili wa serikali Monica Mbogo aliyekuwa akisaidiwa na Beatrice Mpangala
Dudu aliwaeleza washitakiwa hao kwamba kwa mujibu wa kosa linalowakabili hawatakiwi kujibu chochote na kwamba kosa hilo halina dhamana kwa sababu hiyo mahakama haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo isipokuwa Mahakama Kuu. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Februali 10 mwaka huu, itakapotajwa.na wsshitakiwa wamerejeshwa rumanade.
Kesi hiyo ilionekana kuwa na mvuto kutokana na wananchi wengi kuingia katika chumba cha mahakama kwa shauku ya kusikiliza kilichokuwa kikijiri kuhusu kesi hiyo.
Swetu alifariki dunia Jumapili asubuhi katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambako alilazwa Ijumaa usiku baada ya kupigwa na watatu wanaodaiwa kuwa ni wanajeshi wa JWTZ, ambapo hadi sasas wamefikishwa mahakamani wawili na mmoja bado anasakwa na polisi. mwili wa marehemu Swetu ulizikwa jana kwenye makaburi ya Kisutu jijini Dar.
CIAO
JK SAFARINI USWIS

RAIS Jakaya Kikwete, aliondoka nchini jana mchana kwenda Davos, Uswisi kuhudhuria kikao cha kila mwaka kuhusu uchumi (World Economic Forum).
Kwa mujibu wa taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, jijini Dar es Salaam, kikao hicho kitakachoanza kesho na kumalizika Januari 30, mwaka huu, kinahudhuriwa na viongozi wakuu wa nchi, wachumi, viongozi wa mashirika mbalimbali, wanataaluma, viongozi wa dini na wanaharakati mbalimbali duniani.
Baada ya kikao cha Davos, Rais Kikwete ataelekea Addis Ababa, Ethiopia kuhudhuria kikao cha kila mwaka cha Wakuu wa Nchi za Afrika, kitakachoanza Januari 31 hadi Februari 2, mwaka huu na kurejea nchini.
MAUNDA ZORRO a.k.a 'MAMA KIJACHO'

Blog hii ya Chachandu Daily, inamtakia kila kheri dada huyi, Inshaallah, mwenyezi mungu amjalie ampe afya nzuri aweze kujifungua salama mtoto mwenye afya njema
DCDM EAST AFRICA JOINS BDO, THE WORLD'S FIFTH BIGGEST AUDITING FIRM
BDO LOGO
mdau wa BDO
STORY
DCDM East Africa, the fifth biggest accountang and auditing firm in Tanzania has become a member firm of BDO International, the world’s fifth largest auditing firm and will now be known as BDO International. By becoming a BDO member, the firm joinsd others around the world in network spanning more than 115 countries and nearly 1,100 offices
Speaking un Dar es Salaam at press conference to mark the occasion and announce their new name and logo, DCDM East Africa Partner Chanyera Lukumbo, Said “ This isi truly an exciting time in our history as we join a truly prestigious organization. BDO International is renown for uts performance and credibility around the world and by becoming a member firm DCDM East Africa is poised to elevate its position both in the country and in all the markets we operate. This is clear testimony to the record we have and commitment we pit to our work.”.In the thirteen years DCDM East Africa has been operating in the country it has carried out work of national impontance inb servelfields including consulting in civil services reforms in mninistries and parastatals, privatization for Tanzania with reviw of the PSRC, a forensic study on behalf ot TRA and Investment promotion for Tanzania with DBSA and MIGA.
“As part of BDO we will now have access to extensive resources inclundind technology, expertise, training and personnel. It also means that we will be recognized among the world’s most respected entities and even more importantly oir work will carry it our commitment to serve the Tanzanian market better and more eagerly”, added Lukumbo.
BDO was foind inm 1963 as a group firm from US, Canada, The Netherlands, Germany and UK merge with the aim of providinmg better services to their customers. From its inception, the firm was known as Bider Seidman International Group until 1973 when it changed name to BDO. Today the audit and accounting firm has a workforce of more than 44,000 with around 1,100 offices in 115 coutreies around the world.
CIAO
LIGU KUU YA VODA; TOTO AFRICA YADUNDWA NA AZAM FC 1-0
Jan 26, 2010
ZIARA YA DK. SHENI KENYA


Mke wa Makamu wa Rais Mama Mwanamwema shein akizungumza na Mke wa Makamu wa Rais wa Kenya Mama Paulina Kalonzo, walipokutana kwenye chakula cha jioni katika Hoteli ya Intercontinantal mjini Nairobi jana usiku, ambapo Makamu wa Rais Dk. Ali Mohamed Shein yupo Nchini Kenya kwa ziara ya siku tatu.
RAIS SIRLEAF AGOMBEA TENA LIBERIA!!!!!!!
Rais wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf (Pichani) anasema ana nia ya kugombea kwa mara ya pili, licha ya kuahidi kutumikia nafasi hiyo kwa kipindi tu kimoja cha miaka sita.
Rais huyo mwenye umri wa miaka 71 amesema anataka kumaliza dhana zinazotolewa juu ya nia yake ya kugombea mwaka 2011.
Msemaji wake Cyrus Badio amesema hakugundua kulikuwa na kazi kubwa ya kutekeleza kabla ya mwaka 2005, katika nchi inayojaribu kurejesha hali yake ya awali baada ya kuwepo kwenye vita kwa muda mrefu.
Sir Leaf ni mwanamke wa kwanza kuchaguliwa kuwa Rais barani Afrika.
AAlishinda kwa 59% ya kura zote katika marudio ya uchaguzi dhidi ya mchezaji soka maarufu George Weah.
Source http://www.bbcswahili.com/
Rais huyo mwenye umri wa miaka 71 amesema anataka kumaliza dhana zinazotolewa juu ya nia yake ya kugombea mwaka 2011.
Msemaji wake Cyrus Badio amesema hakugundua kulikuwa na kazi kubwa ya kutekeleza kabla ya mwaka 2005, katika nchi inayojaribu kurejesha hali yake ya awali baada ya kuwepo kwenye vita kwa muda mrefu.
Sir Leaf ni mwanamke wa kwanza kuchaguliwa kuwa Rais barani Afrika.
AAlishinda kwa 59% ya kura zote katika marudio ya uchaguzi dhidi ya mchezaji soka maarufu George Weah.
Source http://www.bbcswahili.com/
Subscribe to:
Posts (Atom)