Breaking News

Your Ad Spot

Mar 13, 2011

MAMBO MAMBO BONANZA LA WAFANYAKAZI WA VYOMBO VYA HABARI YALIVYOKUWA

Klab ya Cine iliyopo,  kandoni mwa ufukwe wa Bahari ya Hindi, eneo  la Msasani jijini Dar es Salaam, Jumamosi hii, hapakutosha wakati waandishi wa habari na wafanyakazi wengine wa vyombo vya habari walipojimwaya -mwaya kwenye eneo hilo katika Bonanza la kukata na shoka ambalo hufanyika kila mwaka kwa maadalizi ya TASWA. Mengi yalijiri lakini kwa uchache Chachandu Daily, imekuletea haya.....

Salum Kubenea wa MwanaHalisi akimtoka beki wa TBC 1, Joseph Msami, timu hizo zilipomenyana katika moja ya michuano ya soka ya ufukweni katika bonanza hilo. TBC illala kwa penalti 3-2 baada ya kutoka sare ya bao 1-1.
Hawa bila shaka unawafahamu, ni mtaalam wa 'Amplifaya' ya Clouds FM,  Milady Ayo na mtaalamu mwenzake  Anselim Ngaiza  aka Sog dog... ambao walikuwa kamili pia kwenye Bonanza hiyo.
Hawa siwezi kuwataja majina, lakini ukiwajua nitumie kupitia maoni, Hapa wanasakata muziki wa Twanga Pepeta.
Wadau wakibadilishana mawazo, wakati burudani ikiendelea
Ni kusakata ngoma kwa kwenda mbele
Mzee wa Chachandu Daily hapo vipi? akiuliza mwanadada huyu alipokutana na mtayarishaji wa Chachandu Daily kwenye kona kona  fulani kwenye bonanza hiyo.

Watoto wa miongoni mwa wafanyakazi wa vyombo vya habari, wakijinafasi kwenye eneo maalum la michezo kwenye bonanza hiyo.
Wadau kutoka Uhuru Publications Ltd, wachapishaji wa magazeti ya Uhuru, Mzalendo na Burudani, waki-chat, pembezoni.
Hapa ni Mzee wa Chachandu Daily (kushoto) akiwa na wadau Athumani Hamis, Amina Molell na Faza Kidevu, mbele aya kamera
Hawa ni jamaa wa TBC...yaaani kwa raha zao kama hivi
Mtu kati kama hivi kusakata ngoma...
Ni muziki kwa kwenda mbeleee kila mtu kwa mtindo wake wa kusakata......
Kwenye Kona nyingine wakawa wamepozi, Angel Akilimali wa Uhuru FM na mwenzake........
Sufian Mafoto akisakata muziki na wadau... kama unamuona vizuri hapa mabegi yake yak hakuyaacha...
Wakati wengine , wengine walikuwa wakifuatilia kwa macho huku wakipunga upepo mbele ya 'kilaji' bila shaka hawa si wageni machoni mwako. Kushoto kabisa ni Mheshimiwa Dach wa Channel Ten naye alikuwepo.
Midamida ya jioni hivi, wengine wanatoka na wengine wakawa wanaingia.....
Waooo! ee Fauma.... siku nyingi sijakuona. baadhi waliweza kusema maneno kama hayo baada ya kukutanishwa na bonanza hilo, wakiwa wamepotezana kwa siku kibao,
Twangapepeta ndio waliokuwa wakitumbuiza kwenye onanza hilo

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages